ILIPOISHIA:“He! we Jamal una kichaa nini? Yaani unataka kumwambia nini baba yako? Sasa naona unataka kuuwasha moto ambao kuuzima hutaweza. Ehe! na ukisha mwambia unatarajia nini?” Aliongea mama mdogo kwa kufoka. “Natarajia vyovyote itakavyokuwa, liwalo na liwe.” Alijibu Jamal. Mama yake mdogo alishindwa kuelewa Jamal amepatwa na maswaibu gani akasema.
INAPOENDELEA:“Kwani
kuna nini kilichokufanya ukafikia uamuzi huo mpenzi wangu?” Alihoji mama mdogo. “Sikiliza
kwa makini sana. Mimi siwezi kuendelea kuwa mjinga kiasi hiki. Haya mambo
lazima niyaweke wazi. Nitaishi kwa wasiwasi hadi lini?” Aliongea
Jamal kwa uchungu na kuondoka. “Hivi
Jamal anataka kuwa kichaa au? Yaani amwambie Mzee Said kuwa mimi na yeye
ni wapenzi na tumezaa mtoto? Sidhani kama atakuwa mzima hili ni
tatizo.” Aliwaza mama mdogo. Siku
zilivyozidi kwenda Jamal alikuwa akiota ndoto za kutisha sana.
Mara nyingi
alikuwa akimwona mama yake akimwambia aseme ukweli wa mambo yote
yaliyotokea. Aliishi kwa shida sana, kwani hata usingizi alikuwa
hapati. Hatimaye alianza kuwa mlevi ili asahau ndoto anazoota hivyo
alianza kunywa pombe sana na kutumia dawa za kulevya kama bangi kwa nia ya
kupoteza mawazo. Kumbe ndiyo alikuwa akizidi kuharibikiwa.
Baada ya
kuwa mtumiaji wa vilevi alianza kufeli sana katika masomo yake ya chuo na
baadaye akiwa mwaka wa tatu aliacha chuo na kuanza kuzurula mitaani.
Kutokana na hali yake ya kutumia dawa kukithiri, baba yake alihuzunika
na kuchukia sana baada ya kupata taarifa ya matatizo aliyopata mtoto
wake. Huko
nyumbani mama yake mdogo alikuwa na mawazo sana kwani alikuwa
anatamani sana kumwona Jamal na hasa alipopata taarifa za kuwa
anavuta bangi.
“Jamani ni
kitu gani kimempata Jamal? Mbona alikuwa mzima tu na hajawahi
kutumia dawa za kulevya? Inabidi leo baba yake akirudi nimwambie
amtafute popote alipo ili arudi nyumbani.” Aliwaza mama mdogo. Baada ya
muda mfupi baba Jamal alifika na kumkuta mkewe amekaa chumbani. “Vipi mke
wangu mbona unaonekana mnyonge sana leo?” Aliuliza baba Jamal.“Unajua
baba Jamal mimi nashangaa kwanini huhangaiki kumtafuta mtoto wako na
unajua kabisa ana matatizo. Je akifa huko barabarani?” Alihoji mama
mdogo.
“Yaani
mimi nihangaike na mtu aliyejitakia kuwa mwendawazimu? Unanichekesha
kweli. Mimi siwezi kuhangaika naye muache dunia imfundishe
ipo siku atarudi mwenyewe.” Alijibu baba Jamal huku akivua koti lake
na kulitundika. “Hapana
baba Jamal, huyu ni mtoto wako bora umtafute apelekwe hospitali
ili akafanyiwe uchunguzi lazima atakuwa ana tatizo kubwa. Na kama
hautofanya hivyo basi utakuwa una roho mbaya sana!” Alitamka mama
mdogo.
“Sawa basi
nitatafuta watu wamkamate apelekwe hospitali sijui ni kitu gani kimemfanya
atumie hizo dawa, kwa kweli amenikera sana.” Alijibu baba Jamal
baada ya kukaa kimya kwa muda. “Eh! Sasa
lini utawaomba wamtafute?” Aliuliza mama mdogo akiwa na
furaha. “Nadhani
kesho asubuhi nitawatuma vijana wamtafute popote alipo. Ninaimani
watampata tu kwani nasikia huwa anaonekana sana maeneo ya
Kijitonyama.” Alijibu baba Jamal.
Kesho yake
asubuhi baba Jamal aliwatuma vijana waende kumkamata. Wale
vijana walizunguka sana huku na kule na ndipo ilipofika jioni alionekana
maeneo ya studio Kinondoni akiwa amelala chini hajitambui amechafuka
sana. Walimsogelea na kumbeba kisha kumpandisha katika gari
walilokuwa nalo alikuwa ameishiwa nguvu kabisa. Walimtaarifu baba yake kwa
simu na kumpeleka moja kwa moja hadi hospitali ya Muhimbili ambapo
daktari alimchoma sindano na kumlaza katika chumba cha peke
yake.
Baada ya
muda mfupi baba yake akiwa ameongozana na mama yake mdogo
walifika pale hospitali na kuingia ndani katika chumba alichokuwepo
Jamal. Baba yake alipomwona katika hali ile roho ya imani ilimjia. “Masikini
kijana wangu ndiyo amekuwa hivi siwezi kuamini dokta naomba
umsaidie apone.” Baba Jamal alimwambia daktari.
Wakati huo
mama yake mdogo machozi yalikuwa yakimtoka kwa uchungu. “Daktari
fanya lolote na kwa gharama yoyote Jamal apone.” Alisisitiza USIKOSE SURA YA ....17........
mama
mdogo.
Asante kwa hadithi, ni nzuri sana ila unaweka fupi jamani, ongeza kidogo Adela
JibuFutanikweli nifupi Adela sisi wengine tupo mbali hatuwezi kuvipata hivyo vitabu batunafurahi sana unavyotuandikia ubarikiwe
JibuFutaHONGERA DADA MAANA KWA HAKIKA NAPATA KUELIMIKA....
JibuFuta