Mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru
kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema
aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake...
Kwa apande wake
,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya
mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili
ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa
na Rais |
Kweli ukiwa nyota, utaonekana kila kona. Twashukuru kuwa umepona, ndilo muhimu kuliko yote, afya yako kwanza
JibuFuta