ILIPOISHIA
Akasogea karibu na baba yake akapiga magoti mbele yake huku machozi yakimtoka. “Baba nimekukosea sana! Nimetenda dhambi kubwa mbele za Mungu pia. Nisipotubu dhambi hii sitapona nitateseka maisha yangu yote…”
Jamal aliongea kwa huruma na huzuni kubwa. Baba yake alimsikiliza Jamal kwa makini na huku mama yake mdogo akimwangalia na kuwaza moyoni mwake ni nini anataka kusema Jamal. Aliingiwa na hofu kubwa sana. JE NINI KINAENDELEA USIKOSE SURA YA .......18..........
INAPOENDELEA:
“Baba
unakumbuka wakati ule mama mdogo alipokupa ule ujumbe ambao ulionyesha
kuwa nimeandikiwa na msichana anaitwa Mary na ukanichukia sana hadi
ukakataa kunipeleka shule.” Alieleza Jamal. “Ndio
nakumbuka Jamal lakini nilishakusamehe mwanangu.” Alijibu baba Jamal. “Baba
haikuwa kweli zilikuwa ni njama za mama mdogo kwani alikuwa akinitaka
kimapenzi nilipokataa ndipo akanitafutia sababu nyingi ili unichukie.”
Aliongea Jamal huku akimwangali mama yake mdogo.
“Hivi wewe
Jamal una kichaa au! Unasema nini?” Alihamaki na kufoka mama mdogo
huku akisimama kumfuata Jamal kwa hasira. Baba Jamal
alimtaka anyamaze ili Jamal aendelee kuzungumza. Jamal alisimulia
matukio yote yaliyotokea kuanzia mwanzo hadi mwisho. “Naomba
unisamehe baba haikuwa kusudio langu. Kibaya zaidi baba…” Jamal
alishindwa kuendelea baada ya mama yake mdogo kumkonyezakuashiria
asiseme.
“Eleza
yote mwanangu. Eh! Kibaya zaidi nini?” Aliuliza baba yake. “Kibaya
zaidi hata huyu mtoto Rama si…” Mama mdogo alimziba mdomo
Jamal.
Baba Jamal
alisimama na kumpiga kibao mama mdogo hadi akaanguka chini. “Mwache
aseme yote, kama siyo kweli kwanini unamzuia asiseme?” Alifoka
baba Jamal huku amemkanyaga mama mdogo. Aisha alimkimbilia Rama na
kumchukua na kwenda naye nje. “Baba hata
huyu mtoto si wako nilimpa mimba mama mdogo kipindi kile uliposafiri
miezi miwili. Nakuomba unisamehe sana baba.” Aliongea Jamal huku
ameshika miguu ya baba yake na kulia kwa uchungu.
“Hivi wewe
Jamal umepona kweli au bado unaumwa? Ni mambo gani haya
unayoyasema? Siamini! Utakuwa haujapona vizuri Jamal, mambo haya ni
mazito sana, mwanangu.” Aliongea baba Jamal huku akimwangalia Jamal na
kisha mama mdogo. “Naongea
kweli kutoka moyoni,, baba naomba unisamehe. Nakuomba umuulize
mama mdogo aseme ukweli ulivyokuwa.” Alimaliza kuongea Jamal. Baba Jamal
alimgeukia Jamal na kumpiga kibao ambacho kilimfanya ahisi kizunguzungu
na kuanguka chini huku anapiga kelele.“Ananiua!
Ananiua!.” Jamal alilalamika.
“Nyamaza
mpumbavu mkubwa wewe!” Alifoka baba Jamal. Kisha
alimshika mkono mama mdogo na kumuuliza yote aliyosema Jamal kama ni ya
kweli. “Nakuuliza
wewe kinyago anayosema Jamal ni ya kweli?” Alifoka baba Jamal huku
midogo ikimchezacheza kwa hasira. “Ni kweli!
Naomba unisamehe.” Alijibu mama mdogo huku akitetemeka mwili
mzima. Baba Jamal
alimpiga mama mdogo vibao visivyo na idadi kimyakimya bila kusema
neno lolote. Wakati mama mdogo akiendelea kupokea kipigo, Jamal
alinyanyuka kisirisiri na kukimbilia nje.
Baada ya baba Jamal kumpiga sana mama
mdogo aliingia chumbani na kufunga mlango kwa ndani. Akiwa
ndani alichukua karatasi mbili moja aliandika ujumbe ufuatao na kuweka juu
ya meza: “Mungu
nisamehe Siwezi
kuvumilia hii aibu Naomba
uipokee roho yangu.” Karatasi
ya pili akaandika ujumbe mwingine na kuiweka katika moja ya suruali
zake na kutupa chini ya uvungu wa kitanda. Alipomaliza kuandika ujumbe
alielekea katika kabati lake na kuchukua bastola yake kisha kuielekeza
kifuani na kuifyatua.
Mama mdogo
aliposikia mlio wa bastola aliinuka na kuelekea chumbani na kukuta
mlango umefungwa. Mama mdogo alimwita Jamal na Aisha haraka
ambao walikuwa nje wakiendelea kulia. Jamal na Aisha waliingia na kukuta
mama yao mdogo akihangaika kumwomba baba yao afungue mlango. “Baba
fungua! Baba fungua mlango!” Aliita Jamal. Wakati
Jamal anaendelea kumwomba baba yake afungue mlango, Aisha aliendelea
kumbembeleza Rama ambaye muda wote alikuwa akilia. Mama mdogo
aliamua kukimbia na kutokomea kusikojulikana.
Jamal
aliamua kupiga simu polisi ambao walifika haraka na kuvunja ule mlango na
kumkuta baba Jamal akiwa amelala pale chini tayari alikuwa amekufa.
Jamal na Aisha walilia sana huku wakimkumbatia baba yao kwa uchungu.
Polisi walianza kuhoji chanzo cha tafrani ile, Jamal alipoanza kueleza
ndipo alipogundua kuwa mama mdogo hakuwepo. Wote walianza kumtafuta
mama mdogo katika vyumba vyote lakini hakuonekana. Walikwenda
nyumba za jirani hakuwepo. Ikawa ni tafrani mpya ya kumtafuta
mama mdogo hadi apatikane.
Umati wa majirani na watu kutoka
mitaa mbalimbali ulizingira nyumba ya akina Jamal ili kujua kulikoni.
Pamoja na umati mkubwa wa watu kusaidia kumtafuta mama mdogo
hakuweza hakupatikana. Polisi waliamua kuuchukua mwili wa baba Jamal
wakati uchunguzi wa chanzo cha tukio ukiendelea. USIKOSE SURA YA 19.........
This is very useful for me.Can you share with us something more like this. Thanks.
JibuFutaThis is very useful for me.Can you share with us something more like this. Thanks.
JibuFutaNatafuta 19 na 20 mbona sioni ?
JibuFuta