ILIPOISHIA“Jamani za siku nyingi.” Aliendelea kumsemesha
Julieth. Mwanzo Julieth hakumtambua lakini alivyozidi kumwangalia akamkumbuka.
“Oh! Kumbe Zubeda! Mambo vipi rafiki yangu?
Nimefurahi sana kukuona habari za hapa?” Zubeda alikuwa ni rafiki yake Julieth,
kwani walikuwa wakiuza chapati pamoja wakati Julieth akiwa Arusha. Domina alianza kulia, haraka Zubeda alimchukua
Dominiki ili Julieth amnyonyeshe Domina. USIKOSE SURA YA 11
INAPOENDELEA
“Habari za hapa ni nzuri kiasi.” Aliongea Zubeda huku
akimshika vizuri mtoto.
“Nzuri kiasi!” Alihamaki Julieth huku akimkazia macho
Zubeda.
“Ndiyo! Nzuri kidogo.” Alisisitiza Zubeda huku
akiyakwepa macho ya Julieth.
“Vipi mwenzangu
mbona ulikuwa kimya sana? Wakati mama yako akiwa anaumwa tulikupigia simu mara
nyingi lakini haikupatikana na …”
“Ehe! Sasa anaendeleaje?” Julieth alimkatisha Zubeda
na kuuliza akiwa katika hali ya kushtuka.
Zubeda
aliwachukua watoto wa Julieth na kukaa nao pembeni wakati yule dereva
akiondoka. Julieth alitaka kuingia ndani moja kwa moja lakini Zubeda alimzuia.
“Julieth
wadogo zako na mama yako hawapo hapa.” Zubeda alianza kueleza.
Kama nilivyokudokeza mama yako aliugua sana,
tulikutafuta kwenye simu yako ili utume fedha za matibabu bila mafanikio. Kwa
vile mama yako alikuwa hana pesa ikabidi auze simu yake ili apate pesa za
matibabu.”
“Oh! Samahani sana. Simu yangu iliharibika nikawa na
simu nyingine. Lakini namba ya mama ninayo, ila nilishawahi kumpigia lakini
haikupatika. Labda ndo kipindi
alipoiuza. Aliongea Julieth kwa masikitiko.”
“Lakini mbona
hata mume wako tulimpigia simu hakupokea, tuliamua kumtumia ujumbe lakini
hakujibu. Hivi kwa nini mlikuwa mnafanya hivi?” Aliendelea kuhoji Zubeda huku
Julieth akimsikiliza kwa makini sana.
“Ni histora ndefu hebu nitulie kwanza nitakusimulia
siku nyingine wewe ni rafiki yangu sitakuficha kitu. Eh! Hebu niambie mama na
wadogo zangu wanaishi wapi sasa?” Julieth alihoji zaidi.
“Wadogo zako
waliondoka kutokana na kushindwa kulipa kodi ya nyumba, kwa sasa sijui watakuwa
wapi.” Alijibu Zubeda.
“Eh! Na mama?. Aliuliza Julieth.
Zubeda alimwangalia usoni Julieth ambaye alikuwa
akionyesha uso wenye maswali mengi sana. Kwa muda wa dakika moja hivi Zubeda
aliwaza na kutaka kumdanganya Julieth kuhusu aliko mama yake. Lakini mwisho
aliamua kumwambia ukweli.
“Baada ya kuugua kwa muda mrefu mama yako ali…”
Alisita kidogo Zubeda.
“Alifanya nini?.” Julieth aliuliza.
“Alifariki dunia.” Zubeda alijibu huku akimpa pole Julieth.
Julieth aliyekuwa amesimama alipiga kelele na
kuanguka chini puu! Huku nguvu zikimwishia. Alilia sana kama mtoto aliyeungua
moto.
“Mamaaa! Mamaaa!
Mama yangu wee! Upo wapa mama! Siamini nipeleke nikamwone. Nipeleke! Nipeleke!”
Aliendelea kulia, kugagaa chini na kutamka maneno mbalimbali kwa uchungu sana.
Hata hivyo haikusaidia kitu mama yake alikuwa ameshafariki na kuzikwa siku
nyingi sana.
Julieth
alikuwa ameishiwa nguvu kabisa hivyo Zubeda aliwabeba watoto wote. Ilikuwa
yapata kama saa mbili hivi za usiku, Julieth alinyanyuka kwa nguvu za ajabu na
kugonga geti la nyumba aliyokuwa akiishi mama yake huku akiita ;
“Mama fungua mimi mtoto wako Julieth nimerudi.”
“Hapo kuna mpangaji
mwingine Julieth unawasumbua watu bure.” Zubeda alimkataza Julieth. Lakini
Julieth hakutaka kumsikiliza. Kutokana na geti kugongwa kwa nguvu alitoka kaka
mmoja na kufungua.
“Vipi dada una matatizo gani?” Aliuliza
yule kaka.
“Yuko wapi mama yangu, namtaka mama
yangu.” Aliuliza Julieth huku akilia na akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa.
Yule kaka hakumwelewa anachozungumza akabaki
anamshangaa. Ghafla Julieth alianguka chini na kuzimia. Yule kaka na Zubeda
walisaidiana kumnyanyua Julieth na kumwingiza ndani kisha wakamlaza chini huku
feni ikimpepea. Yule kaka akamuuliza Zubeda aliyekuwa amewabeba watoto wa
Julieth.
“Vipi huyu
mwenzio ana matatizo gani?” Aliuliza yule kaka.
Zubeda akamwelezea kila kitu yule kaka ambaye ndiye mpangaji
mpya katika ile nyumba, alimwonea huruma sana Julieth. Baada ya Julieth
kuzinduka aliendelea kulia asijue nini cha kufanya kwa yote yaliyomkuta. ITAENDELEA SURA YA 12......................
mmmh! jamani very sad!
JibuFutaSo sad jamani...... Mungu akupe nguvu na afya njema uendelee kutupa burudani sambamba na kutuelimisha. wasimuliaji wengine au wamechoka au hawataki tu kutusimulia bali wewe pamoja na umri wako mdogo Mungu akuongoze uzidi kutupa raha mpendwa
JibuFuta