Pages

Jumanne, Machi 26, 2013

SIMULIZI YA KUSISIMUA,,, BADO MIMI SURA YA .......1......

“Napata  maumivu makali sana jamani naombeni mnisaidie nateseka sana eeh Mungu wangu” ilikuwa ni sauti ya  Mama kutoka chumbani niliinuka na kukimbilia ndani huku nikimwangalia Mama kwa huzuni kutokana na maumivu ya tumbo aliyokuwa akiyasikia nilisogea karibu “Pole mama twende nikupeleke Hospitali” Alijivuta kidogo na kuinua uso wake huku akinitazama “Mwanangu baba yako yuko wapi”  Nilimshika mama mkono “Baba ametoka ameenda kazini”.

 Kutokana na hali aliyokuwa nayo Mama nilitamani kumsaidia lakini sikuwa na namna kwani maumivu aliyokuwa anayapata yalikuwa makali sana “Kandida mwanangu naomba umtafute Baba yako anipeleke hospitalini” Baba yangu alikuwa ni mfanyakazi katika kiwanda cha plastiki na Mama alikuwa hana kazi nikiwa ni mtoto wa kwanza katika familia yetu na wadogo zangu wawili ambao wote walikuwa wakisoma shule ya msingi wakati huo mimi nilikuwa kidato cha pili pale nyumbani hakukuwa na mtu yeyote zaidi yangu na Mama alikuwa ni mgonjwa, hali ya mama yangu ilizidi kuwa mbaya ikanibidi nikimbie kwenda kumuita jirani yetu anayeitwa  Mama Keku.

“Mama keku ,Mama keku” Niliita kwa sauti kubwa iliyojaa wasiwasi mwingi “hee kuna nini Kandida  mbona  unaita kwa sauti kali hivyo” Alinijibu mama keku  huku akitoka chumbani kwake wakati huo machozi yalikuwa yakinibubujika kwa wingi “Mama yangu anaumwa, Mama yangu anakufa jamani naomba uje umsaidie tumpeleke hospitali” Niliongea kama nimechanganyikiwa. 

“Sasa mbona sikuelewi,  inamaana amezidiwa yuko na nani nyumbani? Embu twende haraka ukilia haisadii chochote” Tuliondoka haraka nyumbani kwa Mama Keku na kuelekea chumbani kwa mama yangu safari hii tulimkuta Mama akiwa kimya huku macho yakiwa yamemjaa machozi na hata tulipomuita hakuzungumza lolote “Mama yangu jamani Mama uwiiiiiii nisaidie mimi Mama yangu” Nililia kwa uchungu nikijua Mama yangu atakuwa amefariki Mama Keku alitoka nje haraka kwaajili ya kwenda kutafuta usafiri wa kumpeleka Mama hospitali .


 Alirudi akiwa na usafiri wa gari dogo taksi aina ya corolla na majirani walisaidiana kumbeba mama na kumpeleka hospitalini.kulikuwa na umbali mkubwa sana hadi kufika katika hospitalini tulipofika pale wahudumu walikuja na kitanda cha kuwabebea wagonjwa (machela) na kumbeba mama haraka kumpeleka kwa daktari kwa uchunguzi zaidi Mama keku alimpigia simu  Baba na kumjulisha kuwa tulikuwa Hospitalini na hali ya mama Ni mbaya Baba alifanya haraka ili kufika pale hospitalini.

Ilipita kama nusu saa tokea mama aingizwe katika chumba cha uchunguzi Daktari alikuja “anayehusika na mgonjwa ni nani?” aliuliza huku mimi na mama keku tukiwa tunamsikiliza “Mimi ndiye niliyemleta mgonjwa ni jirani yangu na huyu hapa ni mtoto wake” alisema Mama Keku “Hakuna ndugu mwingine wa karibu zaidi ” aliuliza Daktari “Mume wake yupo njiani anakuja alijibu mama Keku  “Akifika mwambie aje anione “Mama yangu anaendeleaje naomba kumuona” Nilimsogelea Daktari na kumshika katika koti lake kwa nguvu kwani nilikuwa kama nimechanganyikiwa sijui nini hatima ya Mama yangu “Usijali mtoto tulia Mama yako anaendelea na matibabu utapata nafasi ya kumuona baadaye. Nini kitaendelea usikose SURA YA PILI......................

Maoni 7 :

  1. Inaendelea lini tena dia

    JibuFuta
  2. Mwanzo mzuri, ila imekuwa fupi xna ktk kipande hicho cha kwanza. Tupia, tupia kitu watu wajifunze ya dunia.

    JibuFuta
  3. iko pouwa ile mbaya

    JibuFuta
  4. asanteni sana wadau tuko pamoja sana

    JibuFuta
  5. Adela, mbona kama ile hadithi ya chungu na tamu ya penzi haijaisha au kuna vipande ambavyo sijaona, maana naona similizi ya mwisho nimeisikiliza imeishia yule dada anapanga kutoroshwa kesho yake arudi Dar baada ya kugundua ngereza ni mchawi, then ikakatika, najaribu kutafuta muendelezo wake sioni. Asante dear simulizi zako ni nzuri sana.

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.