Yawezekana umekuwa na marafiki wengi wanaokuzunguka na kila mmoja ana tabia zake, kuna baadhi ya watu anaweza kuwa karibu na wewe huku akijifanya anafurahia maendeleo yako ama akikusifia katika kila jambo unalolifanya, huku akionyesha kukubaliana na wewe kwa kila jambo, ni wazi kuwa mtu huyu utamuamini na kumuona rafiki mzuri. Lakini wanasaikolojia wanasema "Rafiki wa kweli ni yule ambaye hakubaliani na wewe kwa kila jambo mambo mengine lazima atayapinga" Hata kwenye mapenzi pia utakuta mtu anakusifia, anakuambia maneno matamu unajisikia furaha kumbe mwenzio kuna kitu anakitaka akishakipata wala hakuna mapenzi. NI VYEMA KUWA MAKINI |
Lakini wanasaikolojia wanasema "Rafiki wa kweli ni yule ambaye hakubaliani na wewe kwa kila jambo mambo mengine lazima atayapinga"
JibuFutaHapa tuwe makini pia, angalia hapo `mambo mengine'
mfano, wewe kila ukipika chakula mwenzako anakikosoa...utajisikiaje?
Ni kweli kibinadamu huwezi kuwa `mkamilifu' kwa kila kitu na ili uboreshe inabidi kuwe na mtu mwingine wa `kupima' kama akiona makosa akurekebishe,lakin kwa hekima
Unafiki ni pale mwenzako aone kuna makosa na bado akaendelea kukusifia. Huyu hakutakii mema, na kama mtu wa kuvimba kichwa, wewe utajiona umsafi kumbe umejipaka kinyesi....
Ni hayo kwa leo.