Pages

Jumamosi, Februari 01, 2014

AMA KWELI DUNIA INA MAMBO "MWANADADA AFUNGA NDOA NA WANAUME WAWILI"


Mwanamke huyo pichani  anayeitwa Belinda mwenye umri wa miaka 32, akiwa na mume wake wa kwanza, Yasemekana mwanamke huyu alifanikiwa kufanya udanganyifu huo kwa kushirikiana na Baba yake mzazi.Gazeti la The Finder nchini Ghana liliripoti kuwa mwanamke mwanamke huyo aliolewa na mume wake wa kwanza Maxmus Anumah ambaye ni mfanyakazi wa Hospitali ya kijeshi ya 37 mwaka 2012 kisha kuolewa na mwanamume mwingine  Audrey Atikpo January 2013 huku  akiwa bado katika ndoa ya awali.

Ilielezwa kuwa katikati ya january 2013, Belinda ambaye alionyesha kutofurahishwa na ndoa baina yake na mumewe wa kwanza, alimuomba ruhusa mumewe huyo ya kwenda kwenye kituo cha maombi cha Edumfa kwaajili ya sala ya kufunga ili wapate watoto, ambapo mumewe alikubali ombi hilo.

Huku mumewe akiwa hajui kinachoendelea, Belinda kwa kushirikiana na Baba yake na baadhi ya wanafamilia waliandaa ndoa ya siri ya binti huyo kwa mwanamume mwingine Audrey Atiko ambaye alikuwa amerejea kutoka Marekani na haijafahamika kama waliwahi kukutana awali au la.

Ripoti hiyo ilieleza pia kwa mujibu wa vyeti vya ndoa yake ya pili.Belinda aliolewa na Atikpo January 31,2013 na waliandikisha ndoa hiyo kwenye mahakama ya wilaya ya Somanya.Baadaye  jamaa huyu alikodi nyumba ya makazi kwenye eneo lijulikanalo kama East Legon ambapo aliishi na Belinda kwa muda mfupi kisha kurejea Marekani kwaajili ya kuandaa utaratibu wa kumuwezesha Belinda kuungana naye kwa kwenda nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo baada ya Atikpo kuondoka Belinda alikusanya vitu vyake na kurejea kwa mumewe wa kwanza  katikati ya mwezi wa pili, 2013.Ilielezwa baada ya kurejea huko Belinda alianza kukosoa kila alichokuwa anafanya mume wake huyo wa kwanza na kusababisha mzozo ya kila mara baina yao.

Miezi kadhaa baadaye, baba yake alikwenda kuwatembelea na kusema kuwa Belinda anahitaji apewe talaka, lakini mume wake huyo alikataa kufanya hivyo, Baada ya kupata shaka kuhusu simu za mara kwa mara kwa mkewe kutoka kwa watu tofauti ambazo alibaini zinapigwa kutoka Marekani, Maximus alihitaji kupata maelezo kuhusu simu hizo na Belinda alimwambia kwamba mwanamume ambaye amekuwa akimpigia simu (yaani mumewe wa pili, Atikpo) ni binamu yake na mwanamke ambaye amekuwa akiwasiliana naye (yaani mama mkwe wake aliyeko Marekani) ni shangazi yake.

Kwakuwa hakuridhika na majibu, Maximus aliamua kuanza kumfuatilia kimya kimya na katika juhudi hizo alibaini kipande cha karatasi, kilichokuwa chumbani kwao kikiwa  na jina na anauani ya Atikpo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jamaa aliamua kutumia mtandao wa facebook kutafuta jina la Audrey Atikpo kisha kumtumia ombi la kuomba urafiki. Baada ya kukubali  ombi hilo na kisha kuona picha ya harusi ya Belinda na mume wake wa kwanza kwenye ukurasa wa facebook, Atikpo alianza kumshambulia Maximus kwa ujumbe mkali ambaye kila mmoja alieleza kwamba ndiye mume halali wa Belinda.

Kwa mujibu wa The finder, siku iliyofuata Atikpo alimpigia simu Belinda kutokea Marekani na kumuuliza kuhusu suala hili, ambapo Belinda aliamua kukusanya kila kilicho chake kutoka nyumbani kwa mume wake wa kwanza na kwenda kwenye nyumba aliyokuwa amepangiwa na Atikpo. MMMH YAANI HILI NI BALAA, AIBU GANI HII CHANZO. MWANANCHI..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.