Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema tukio hilo la kinyama
lilitokea mwanzoni mwa juma huko katika Kijiji cha Kisa wilayani
Sumbawanga mkoani Rukwa.
Taarifa zilizotolewa na polisi wilayani
humo zilisema, mwanamke huyo alikuwa mke wa mtu na aliwahi kumtoroka
mume wake na kwenda kuishi na mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la
Josephat Chinga (32) na siku chache baadae nako kwa mpenzi wake huyo
hakuonekana ghafla na baadae ndipo alikutwa ameuawa.
Kamanda
Mwaruanda alisema, kichwa cha mwanamke huyo kilikutwa ndani ya sufuria
na pemezoni kulikutwa karatasi lililokuwa na ujumbe ambao baada ya
kusomwa iligundulika iliandikwa na mmoja wa wauaji.
Mtu
aliyeandika barua hiyo alifafanua aliandika ujumbe huo baada ya
aliyewatuma kumuuwa mwanamke huyo kushindwa kuwalipa ujira
waliyoahidiana hivyo kuamua kumlipua na kuorodhesha majina ya wote
waliofanikisha mauaji hayo.
Mtu huyo alifafanua kwua aliyewatuma
alikuwa na lengo la kuchukua viganja vya marehemu huyo kwani alikuwa na
faida navyo kwa kuwa ilisemekana vilikuwa na alama ya ‘M’ angevipata
angetenezea dawa ya utajiri.
Mtu huyo alifafanua kuwa, waliahidiwa kulipwa shilingi laki nne kila mmoja aliyefanikisha mauaji hayo.
Kufuatia tukio hilo tayari watu wanne wameshakamatwa na wako mikononi mwa jeshi la polisi |
|
|
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.