Pages

Jumamosi, Machi 22, 2014

MDAU "MAVAZI FILAMU ZA BONGO NI AIBU'


Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa filamu za hapa nyumbani, lakini naanza kukata tamaa kuziangalia kutokana na mavazi yanayoonekana kuwaacha wanawake nusu utupu. Nakosa raha haswa ninapoangalia filamu hizi na familia yangu. Nikiwa kama mzazi, naona watoto wangu pia watajifunza  na kuiga aina hiyo ya mavazi. Wakati mwingine mazingira hayana ulazima kwa mhusika kuvaa nguo ya kuacha maungo yake wazi, lakini kwakuwa ndiyo hulka yao, basi imekuwa ndiyo mtindo sasa. Jamani mnapaswa kubadilika na kuangalia utamaduni wetu wakati wa uandaaji wa filamu zetu tusiige kila kitu kutoka katika mataifa ya wenzetu, tukumbuke mila na desturi zetu. BY BABA TUNU MKEREKETWA DAR  ES SALAAM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.