Mwanasiasa Mkongwe na Mbunge wa viti maalumu Anna Abdalah amesema "Lazima wanawake wajengewe uwezo, Tunataka nchi inayojali usawa wa kijinsia, hatutaki kusikia maneno ya kejeli, kwa wanawake wanaojitokeza kugombea uongozi kwa lengo la kuwavunja moyo ili warudi nyuma. Kuna umuhimu kwa vyama vya siasa kuwa na demokrasia ya kweli kwani kwa kufanya hivyo mfumo wake wa uendeshaji kamwe hauwezi kujali usawa wa kijinsia.
Pamoja na hayo amesema ataendelea kupambana na kukemea vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake wanaotafuta uongozi. "Ndani ya siasa wanawake wananyanyasika kwa kukumbana na kauli chafu na maneno ya kejeli kuwa hawawezi uongozi, utasikia mtu anasema wewe utamchaguaje mwanamke ambaye anachuchumaa wakati wa kwenda haja" Haya si maneno mazuri mtu wa namna hiyo anamdharau mwanamke ambaye ni sawa na Mama yake mzazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.