Pages

Jumatatu, Machi 31, 2014

WANAWAKE WANAWEZA,,,,,WAKATI WOTE

Hapo zamani ujumbe ulikuwa "Wanawake  wakiwezeshwa wanaweza" sasa msemo huo umeboreshwa  na si wakiwezeshwa ndiyo wanaweza bali "Wanawake wanaweza wakati wote" (wwww). Wanawake wa sasa wamesonga mbele katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kiuchumi kibiasahara, kisiasa na kijamii, kiutamaduni , kimazingira kiteknolojia, kisayansi na katika nyanja nyingine nyingi ambazo wamefanya vizuri bila hata kuwezeshwa  kwa maana ya kwamba wamejiwezesha wenyenyewe.

 Kutokana na hali hiyoumefika wakati wanawake wanapaswa kuchochea mabadiliko katika kuleta usawa wa kijinsia yaani kuhimiza usawa wa mwanamke na mwanaume katika nafasi mbalimbali ili kupata mafanikio katika maisha yao.Amesema Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) Tanzania, Dr Fatma Mrisho. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.