Wauguzi na watendaji wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii wametakiwa kuhakikisha wanawafichua pamoja na kuwakemea wanaotoa maneno ya kuudhi kwa wagonjwa hasa wajawazito.Kumekuwa na taarifa mbalimbali zikielezea tabia ya baadhi ya wauguzi, kutoa maneno ya kuudhi kwa wagonjwa kitu ambacho siyo kizuri kwani kinahatarisha usalama wa afya ya mgonjwa. Hayo yamesemwa Siku ya jana na Waziri wa Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dr. Seif Rashid alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa 15 wa wauguzi na wakunga binafsi jijini Dar es salaam jana.Dr Rashid amesema Serikali imejipanga kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha inapunguza vifo vya wajawazito na watoto ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.