Kwa mtazamo wangu hakuna haja ya serikali tatu ni vyema kubaki na serikali mbili. Kwani kuingia kwenye serekali tatu nikuibua mpasuko zaidi utakaokuwa muungano, lakini ppia ikiwa ni kujiongezea mzigo katika maisha. Na yote hii ni kwasababu gharama za kuhudumia serikali zitakuwa kubwa huku nchi yetu ikiwa na matatizo mengi yanayokosa ufumbuzi. Badala ya kutumia fedha kidogo tulizonazo kugharamia serikali tatu ya Tanganyika na Zanzibar ni bora, zitumike kuimarisha huduma za jamii. Ushauri kwa wananchi ni kwa mba tuendelee kujielimisha zaidi juu ya umuhimu wa mapendekezo mengine katika rasimu ya katiba badala ya kung'ang'ania eneo la muungano tu. Mwisho ni kwa wajumbe wa Bunge maalumu la katiba nao waache kuligeuza bunge letu kuwa jukwaa la malumbano yanayofanana na maigizo kila siku.
Kila maoni yana umuhimu wake, na ingelifaa kama ingeliwezekana kila Mtanzania angelitoa maoni yake. Ndio maana kwa mtizamo wangu, hili swala kama lina utata, basi lirudishwe kwa wananchi walipigie kura, ili kila mtu awe amewajibika.
JibuFutaKwa maoni yangu, vipengele kama hivi vyenye utata, viachwe kwanza kwa ajili ya hizo kura za wananchi.
Muda ni muhimu sana, na mambo yapo mengi, ningelionelea kwa mtizamo wangu, wajumbe waendelee na vipengele vingine, mwisho wa siku watavirudia vipengele vigumu na kutoa maamuzi ya pamoja kuwa haya yanahitajia kura za wananchi.