Kwa mujibu wa jarida la Health living kabichi ina uwezo wa kuzuia na kukabiliana na magonjwa mbalimbali nyemelezi kwa ubongo, Vilevile kabichi inatajwa kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake. Inaelezwa kuwa tishu zilizopo ndani ya mboga hii huzuia kukua kwa kasi ya ugonjwa wa saratani ya matiti.
Kwa wenye tatizo la kuumwa kichwa mara kwa mara supu inayotokana na kabichi iliyochemshwa ni dawa inayoweza kukabiliana na hali hiyo ndani ya muda mfupi. Kwa wale wenye ngozi yenye mafuta na kushambuliwa na chunusi sugu kabichi ina uwezo wa kukausha mafuta na kuiacha ngozi ikiwa kwenye hali ya ukavu.
Kabichi pia inatajwa kuwa kichocheo katika mzunguko wa damu na kuifanya itiririke na kuzunguka vizuri katika mishipa ya damu. Pia supu ya kabichi inasaidia kupunguza uzito wa mwili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.