Pages

Ijumaa, Aprili 11, 2014

SOMA MKASA HUU ,,MASIKINI EVELINA

Evelina alikutana na Thobias aliyemfahamisha kuwa anahitaji mtu wa kuishi naye kwasababu mke wake ametoroka na kwamba baada ya kutafakari kwa makini alikubaliana naye, Hata na hivyo anasema mume wake huyo alianza pombe kila siku na mara kwa mara na kwamba kila aliporejea nyumbani majira ya usiku wa manane na kumkuta amelala alimuamsha na kisha akawa na tabia ya kumtukana matusi ya nguoni kisha kuanza kumpiga. Aliendelea kuvumilia na kumpenda mumewe kwa imani kuwa siku moja ataacha kulewa na wataelewana kimaisha.

Baadaye waliamua kulima pamoja shamba la korosho katika kijiji cha Nang'imbwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Hata hivyo siku zilivyozidi kwenda mambo yalizidi kubadiliaka na siku moja ambapo ilikuwa ni sikukuu ya pasaka mwaka jana, Siku hiyo mumewe  alikwenda kunywa pombe za kienyeji  na kurejea usiku. Aliporejea na kubaini kuwa yuko katika hali hiyo, aliamua kujificha kwenye chumba cha watoto wake ili kuepusha shari. Akiwa chumbani kwa watoto ilikuwa ni usiku sana baada ya muda mfupi alijihisi kujisaidia choooni.


 Kumbe kwa kufanya hivyo mumewe alimuona na kumfuata kisha akampiga na kumjeruhi mkono na mguu. "Alinifuata akanipiga kwa panga kisha aakanikata mkono na kubaki mfupa mmoja tu. Pamoja na mguu wangu umekatwa nililetwa hospitali tarehe moja mwezi wa nne majira ya usiku...Anasimulia huku akibubujikwa na machozi katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.

 Eveline amesema "Kwa Thobias sitarudi tena baada ya kunikata kwa panga alikimbilia kusiko julikana nahisi anaogopa kukamatwa. Siwezi kurudi kwake tena maana ataweza kuniua kabisa siku moja" Licha ya vipigo hivyo, na kulazwa hospitali Evelina haonyeshi kukata tamaa ya kuolewa tena na mwanaume mwingine akijitokeza. "Nikimpata bwana mwingine nitaolewa maana mimi ni mwanadamu nitaolewa tu, labda mwenyezi Mungu atanisaidia kumpata mume mwenye tabia tofauti". Inasikitisha sana hali kama hii Evelina ni miongoni mwa wanawake wengi katika wilaya ya Ruangwa na sehemu nyingine nchini waliopata vilema na kuteseka kutokana na vipigo kutoka kwa waume zao hata kuchangia ndoa kuvunjika na watoto kubaki bila msimamo kwasababu ya migogoro ya wazazi. 

 Baadhi ya wanaume katika maeneo mbalimbali ya nchi wabaendeleza ukatili wa kijinsia kwa kuwapiga wanawake licha ya kuwa hatua hiyo ni kosa kwa mujibu wa sheria. Chama cha Wanahabari Wanawake Tamwa kimefanya utafiti kuwa vipigo kwa wanawake kwenye ndoa ni ukatili mkubwa  unaoendelea kwa familia nchini. Hata hivyo vipigo hivi huchukuliwa kama vitendo vya kawaida hasa katika maeneo ya vijijini. CHANZO MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.