Pages

Alhamisi, Aprili 03, 2014

TUMIA ASALI NA KARANGA KUSAFISHA USO UPATE MATOKEO YAKE

Chukua unga wako wa karanga na uuchanganye na asali mbichi kiasi kidogo, kisha acha kwa muda wa dakika 10 ili vichanganyike.  Chukua mchanganyiko wako, kisha paka usoni hasa zile sehemu unazoziona kuwa na mikunjo zaidi.
Subiri kwa dakika kama 10, kisha osha uso wako na sabuni isiyo na kemikali baada ya hapo futa uso wako na kitambaa kisafi na kikavu.  Subiri tena kwa dakika 5 halafu paka mafuta au losheni. Unashauriwa kufanya hivi mara moja kwa wiki.
Kiasili njia hii imekuwa ikitumiwa na Wanyamwezi wa Tabora kama kipodozi kwa ajili ya mabinti wadogo pindi wanapokaribia kufanyiwa sherehe maalum.
Unaweza pia kusugua taratibu uso kwa kutumia mchanganyiko wako ili kuondoa takataka katika mwili wako ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo unaweza kujipodoa kwa kupaka aina nyingine za vipodozi.
Kwa kuwa hazina madhara, unaweza kufanya hivi kila siku na utafurahia matokeo yake.

Kwa kazi hii ya ngozi, karanga zinazohitajika ni zile mbichi. Kitu kinachohitajika ni kuchukua karanga mbichi ambazo hazijakaangwa kiasi kidogo kama kikombe kidogo cha chai.
Zianike karanga juani kwa muda ili ziweze kumenyeka kwa urahisi bila kukaanga.  Saga karanga zako kwa kutumia blenda au kitu chochote kitakachoweza kuzilainisha na kuwa unga laini.  

Maoni 1 :

  1. ASANTE SANA KWA KUTUELIMISHA TAFADHALI NAOMBA UNISAIDIE MAFUTA YA ASILI KATIKA MWILI WANGU NATAKA UWE LAINI MAANA NA NGOZI KAVU YAMWILINI ILA USO MASHAALLAH NI WA MAFUTA NATUMIA VIPODOZI ASILI UKO VIZURI.

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.