Ili kufikia malengo, ni vyema kuthubutu na pale unapofanya jambo fulani lazima kutakuwa na watu wengi ambao wanafanya kazi hiyohiyo, kwani siku zote unaambiwa hakuna kazi ya peke yako, mfano kama ni msanii wa muziki lazima siku zote awe mbunifu ili aendelee kufanya vizuri katika gemu la muziki. vinginevyo unaweza kupotea na kazi zako zikabaki kuwa historia.
Vilevile katika kazi yoyote, ni vyema kuwa mbunifu ili kwenda sawa na ushindani, kwani bila kuwa mbunifu ni vigumu kushindana na yule ambaye kila siku anaumiza kichwa kufanya kitu kizuri zaidi, mwisho wa siku unabaki ukilalamika lakini vitendo hakuna. Unaambiwa "Ukitaka ushindani onyesha vitendo, usitumie maneno matupu" |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.