Dalili za ugonjwa wa Dengue ni homa kuumwa kichwa, uchovu na maumivu ya viungo huanza
kujitokeza kuanzia kati ya siku tatu
hadi 14 tangu mtu anapoambukizwa kirusi cha homa hii, Dalili nyingine ni
kutokwa na damu kwenye fizi na puani na chini ya ngozi na iwapo mgonjwa ataumia sehemu yeyote ya
mwili ni rahisi kupoteza damu nyingi kupitia kwenye michubuko lakini wapo
wanaopoteza fahamu wakati mwingine dalili zake hufanana na za malaria .
Kutokana na kutokuwepo kwa tiba ya ugonjwa huu kwa nchi kama za Thailand,
Malaysia na India wameweza kupata kinga na tiba kwa kutumia papai au majani ya
mpapai.
Wanasema ni vyema mtu akala papai pamoja na mbegu zake katika kumsaidia
kujikinga na dengue. Unachukua majani mawili ya mpapai na kuyasafisha vizuri kisha unayatwanga kwa
kutumia kitambaa kisafi halafu unakamua kupata juisi yake ambayo huwa ni sawa na vijiko
viwili vikubwa vya chakula. Ila kwa wale wenye blenda wanaweza kuyasaga majani
hayo kwa mashine hiyo na kuchuja kupata juisi yake.Wataalamu wanatoa tahadhari
kutokuchemsha, kupika au kusafisha na maji ya moto kwani itaondoa nguvu yake pia
wanasema mtu atumie majani tu na si mizizi au shina. Juisi hiyo inaelezwa kuwa
ni chungu sana hivyo unaweza kuinywa hivyohivyo au kuchanganya na asali kidogo.
Chanzo cha kuonekana kuwa papai linasaidia ilikuwa ni mwanafunzi huko Malaysia
kuugua ugonjwa huo na kupoteza damu nyingi. Hivyo rafiki wa baba yake alimpatia
juisi ya papai alilosaga bila kumenya na baada ya sikumbili damu yake
iliongezeka sana na kupata nafuu.Mbali na miujiza ya papai wataalamu wa afya
wanashauri hatua nyingine za kuchukuliwa katika kujikinga na ugonjwa huo.
Miongoni mwao nikumaliza mazalia ya mbu kwa kufunika madimbwi ya maji
yaliyotuama na kunyunyuzia viuatilifu
vya kuua viluwiluwi vya mbu, kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalia ya
mbu kama vifuu vya nazi, makopo, matairi ya magari yaliyotupwa ovyo.
Pia
kufyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu, kuhakikisha maua yaliyopandwa
kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama, kufunika mashimo ya maji taka na
kusafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.Vilevile kutumia
viuatilifu vya kufukuza mbu, kuvaa nguo ndefu na zenye rangi ya uangavu ,
kutumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu
na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi. Kujikinga na
homa ya dengue ni rahisi iwapo kila mtu atakuwa makini kumzuia mbu asimuume kwa
kuweka mazingira safi na kutekeleza njia zote za kumzuia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni