Amesema Ugonjwa huo kwasasa ni tishio nchini kwani kwa mara ya kwanza uliibuka mwaka 2010 na watu 30 walipata matibabu, lakini umeibuka tena january mwaka huu na kwamba hadi mwezi huu 369 wameugua na kati yao wawili wamepoteza maisha.
"Watanzania wengi tumezoea tunaposikia dalili za homa kama malaria, tunaenda kununua dawa za malaria, lakini sasa haifai kabisa kwasababu unaweza kununua ya malaria kumbe ni Dengue. Amesema wilaya inayoongoza ni Kinondoni ambayo inawagonjwa 322, ilala 61 na temeke 16. Alisema vifaa hivyo ni vichache, hivyo ni vizuri MSD ikasambaza vifaa hivyo pamoja na dawa ili kupambana na janga hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.