Tazama picha ya mtoto huyu amelala vizuri,,watoto ni malaika hawajui chochote kuhusu dunia na mambo yake.. Huko mkoani Manyara mwanafunzi wa shule ya Sekondari Genda wilayani Mbulu ameshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutupa kitoto kichanga chooni baada ya kuzaa, inadaiwa alitupa kichanga hicho september 23 saa 6.30 mchana. Kichanga hicho kiliokotwa na mtu mmoja kikiwa kizima wakati akipita karibu na choo hicho,,baada ya kukiokota alikipeleka hospitali ya Wilaya,na jeshi lilifanikiwa kumkamata Mwanafunzi huyo. Mwanafunzi huyo alikiri na kusema alifanya hivyo ili aweze kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne utakaofanyika mwezi oktoba... Akizungumza na gazeti la Mwananchi Kamanda wa Polisi mkoani Manyara amesema mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani muda wowowte mara baada ya kutoka hospitalini..ambapo hadi hivi sasa amelazwa..
Watoto kama hawa pichani ni watoto wasio na hatia .... Je,,, katika matukio kama haya ambayo huwa yanatokea mara kwa mara nani wa kulaumiwa? je ni mwanafunzi,,jamii,wazazi,,au yule aliyempa mimba...nini kifanyike jamani... |
Jamii ndio ya kulaumiwa zaidi katika hili.:-(
JibuFutaasante Simon,,,elimu inahitajika jamii pia tusaidiane ili kuweza kutokomeza matukio kama haya inawezekana..
JibuFutaMama weeee yaani hata la kusema sina maana naona nimelalamika mno kuhusu kwanini wanafunzi wanaopewa mimba wasairuhusiwe tu kusoma na pia kufanya mitihani yao kama kawaida?Kama ni kero kwa nini kusifunguliwe shule ya wanafunzi wa aina hiyo? Kwa inasikitisha sana kuona hili jambo la mimba za wanafunzi bado linaendelea, Mimi ningesema ni kosa la wote. grrrrrrrr naacha kwani hasira zangu zinaongezeka ......
JibuFutaKitururu kama ulikuwa mawazoni mwangu. Jamii imezidi sana kuogopesha watoto, matokeo yake ndo haya mtu anaona bora mtihani kuliko mtoto.
JibuFutaaiseee!!! kama mi ni mkuu wa kituo ninge amuru aende jela kifungo cha maisha kwa kitendo hicho pia polisi walishughulikie jambo hili kwa undani zaidi !!! asantee!!!
JibuFuta