Pages

Jumamosi, Oktoba 23, 2010

hivii inawezekana kuishi na mwanamume miaka mingi na kupata watoto halafu unadai talaka kwa madai ya kuwa hukuwahi kumpenda mwanamume..

Inapendeza sana familia kuwa na furaha wakati wote, kama ilivyo katika picha ni wengi wanapenda familia zao ziwe na furaha,lakini inatokea wengine wana furaha na wengine hawana furaha.. Kuna  kaka mmoja anaitwa John alikuwa na mke wake wameishi miaka mingi sana na kufanikiwa kupata watoto sita ,kwa sasa mke wake anamuambia hamtaki tena kwa madai kuwa hakuwahi kumpenda hata siku moja mume wake,sasa jamaa akawaza labda mke wake anamjaribu lakini imeonekana mwanamke anamsimamo na hiyo talaka sasa sijui aliwezaje kuishi na mtu asiyempenda hadi kuzaa naye,,kweli mapenzi kizungumkuti,,ushauri wenu wadau je mnasemaje

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.