Jumatatu, Oktoba 25, 2010

Kuwa makini kuepuka Fungus hatari kwa kucha zako.ni muhimu kuwaona wataalamu kama unalo tatizo hili.

Ugonjwa wa Fungus kwenye kucha ni moja ya magonjwa  ya kawaida hasa kwa nchi ambazo hali ya hewa ni ya joto ugonjwa huo ushambulia kucha na kuziacha zikiwa zimekatikakatika ,wapo baadhi ya watu kutokana na aibu wanashindwa kuvaa kandambili au sendoz ili kuficha ugonjwa huo,,kiutaalamu mtu harusiwi kuvaa viatu vya kufunika ili kuepuka kucha kumeguka zaidi

Kuna sababu nyingi zinaelezwa kuwa kichocheo cha ugonjwa kama viatu vya kubana,soksi chafu na unyevunyevu wa maji usipokausha vizuri miguu baada ya kutumia maji ni miongoni mwa mambo yanayoweza kusababisha tatizo hilo,unaweza kujilinda kwa kuhakikisha miguu inakuwa safi muda wote ,kausha miguu mara inapokuwa na maji kwa mfano umetoka kuoga,zingatia usafi wa mwili mzima,epuka kuvaa viatu au soksi mbichi,epuka kuvaa viatu au soksi zinazobana,na usivae viatu muda mrefu bila kuvua pia zingatia kula chakula bora.

Kama una ugonjwa huu wa Fungus ni muhimu kuwaona wataalamu ili kupata matibabu,ni muhimu kutumia dawa zilizopendekezwa na wataalamu,pichani ni moja kati ya dawa hizo kama unalo tatizo unaweza kuitafuta ili ikusaidie.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom