Pages

Alhamisi, Oktoba 07, 2010

Ni mara chache kusikia bibi na babu wameachana katika mahusiaono,,wakishafikia uzeeni.

Tazama picha hii huyu bibi na babu wakiwa  pamoja,,nimeipenda sana hii picha,,watu kama hawa katika safari ya maisha yao wamekutana na misukosuko mingi  sana,,lakini uvumilivu , pamoja na kumuomba Mungu  viliwaongoza na kufikia hatua  hiyo wakiwa pamoja,wamepata watoto,,wajukuu  na hata vitukuu lakini bado penzi linaendelea...katika  maisha yetu ya kila siku ni mara nyingi sana unaweza kusikia fulani na fulani wamefunga ndoa baada ya miezi kadhaa wameachana, na chanzo ni migogoro inayojitokeza katika mahusiano..jamani tujitahidi tudumishe mahusiano tuliyonayo..tena kwa malengo inawezekana kwani hao walioweza wamewezaje..inawezekana kufanya hivyo..labda kifo tu kiingilie kati na hiyo ni kwa mapenzi ya Mungu ..vinginevyo uhusiano wa kudumu unawezekana..

Maoni 5 :

  1. Ndio Adela, ndoa ni kitu chema na cha heshima, na kwa hiyo kinahitaji `kukijua ' ili uweze kusihi vyema na mwenzako. Sasa kama ni kitu muhimu katika maisha, tuwaulize wanandoa juhudi gani wanazifanya `kuijua ndoa kiundani' Mbona taaluma yako unaisoma na kuijua kiundani, kwanini usifanye hivyo katika kuijua ndoa yako, au kwasababu umeoa au umeolewa iantosha....! Utasema wazee wetu walijifunzia wapi, ...walijifunza kwa kuwaendea wazee wao watu mashuhuri na kudadisi hili na lile kuhusiana na ndoa! Fikiria kipindi hicho kulikuwa na unyago, jando, kufundwa nk, haya ni nini?

    JibuFuta
  2. Natamani kizazi cha sasa nacho kingedumu kwenye ndoa kama mababu zetu wa zamani.Lakini siku hizi ndoa jumapili talaka jumatatu ....mweeee Mola tunusuru.

    JibuFuta
  3. Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kama wanandoa wa sasa watatimiza mwaka mmoja. Zamini ilikuwa safi sana, Naitamani zamani.

    JibuFuta
  4. ....Yasinta...umeitamani zamani wakati zamani iko ndani yako?

    Ni wazo tu Adela ila kiukweli ndoa za siku hizi zimejaa ujinga mkubwa!

    JibuFuta
  5. kweli mungu atunusuru,kizazi chetu hakina huruma,wala hakijui vibaya,

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.