Mtazame huyu jamaa anajisaidia haja ndogo ukutani yaani hii inachangia kuharibu mazingira na ukuta kuharibika haraka ni tabia mbaya hii haipendezi bora usogee pembeni jamani,,,mmmh sijui |
Mtazame huyu jamaa anajisaidia haja ndogo ukutani yaani hii inachangia kuharibu mazingira na ukuta kuharibika haraka ni tabia mbaya hii haipendezi bora usogee pembeni jamani,,,mmmh sijui |
Maoni 5 :
kaazi kweli kweli! hivi kama nje kunaonekana hivyo je ndani? kuna usemi unasema usafi huanzia nje au? Kwa kweli haipendizi kabisa na ndio chanzo cha magonjwa .
kweli haipendezi kabisa halafu mbaya kabisa wanaofanya hivyo ni watu wazima wenye akili zao.
ustarabu ni kitu cha bure
watanzania tubadilike!
Tabia za watu kuwa wabinafsi kutojali wengine, kwa mfano lazima ukifanya kitu ujiulize mwenzangu atajisikiaje, je siwezi kumathiri mwenzangu...hii haipo huku kwetu!
Pili sheria hazina makali...kuna wakati walisema mtu haruhusiwi kuvuta sigara hadharani, lakini hii iliongelewa tu bungeni sijui iliishia wapi. Sheria kama hiyo ilitakiwa iendane na hawo wanaokojoa ovyo, kwani madhara yake yanafanana-fanana!
Kuna mtu alisema kabanwa na mkojo, na yupo kwenye daladala, kashuka chini hakuna choo karibu afanayeje, ajikojoleee? nikacheka, nikamuuliza je kama kabanwa na haja kubwa angefanyaje? akacheka!
na kweli ulimuuliza swali la msingi sana.
kama kawaida sheria za tanzania hazifuatwi kabisa sasa sijui tunazitunga ili nini.
@Yasinta asante kipenzi@emu three hahahahaha daah kasheshe tuko pamoja@.kikubwa zaidi sheria ichukue mkondo wake na kama haipo bora itungwe asanteni sana
Chapisha Maoni