Ijumaa, Oktoba 22, 2010

Ni muhimu kuwa na mahusiano mazuri kazini.

Pichani watu wakiwa makini katika kazi huku wakishirikiana,ili uweze kufanya kazi vizuri na wenzako ni lazima pia kujenga mahusiano mazuri na wenzako  kwani kama hauna mahusiano mazuri na wenzako si kwamba kazi itakuwa ngumu kwako lakini pia utakosa ushirikiano katika kazi na hivyo kujikuta unafanya makosa kazini kwasababu hauna ushirikiano.Katika mazingira yetu ya kazi popote pale unapofanya kazi  hakuna ofisi iliyokosa majungu na fitna.Hii ni kwasababu mbali na kufanya kazi kwa ushirikiano,lakini bado kila mtu ana tabia binafsi inayoweza kuwakwaza wengine.


Inawezekana kukabiliana na watu wanaopenda majungu na fitna katika sehemu ya kazi,epuka kusikiliza,kushabikia na kuongea majungu itakusaidia kutengeneza idadi kubwa ya marafiki badala ya maadui.


Maoni 3 :

emu-three alisema ...

Kama matajiri wangelijua hilo wangefaidi sana, kwani mfanyakazi ukimjali ataijali kazi yako kama yake na ukimfanya mtumwa basi mwisho wa siku na yeye atakuwa nani vile???

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

na wafanyakazi wakijitambua inakuwa swafi hata kama mdosi anawafanyia vimbwanga wao wataona kama maigizo/sarakasi wanaendelea kuchapa kazi tu!

ADELA KAVISHE alisema ...

@Emu three tuko pamoja sana@Chacha pamoja sana ni muhimu sana wafanyakazi kuzingatia hilo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom