Pages

Alhamisi, Oktoba 28, 2010

Ni muhimu kuwajibika kutafuta furaha katika uhusiano ulionao,,kila mmoja bila kutegeana.

Inawezekana kuwa na furaha na amani katika ndoa au uhusiano ulionao kama wote wawili mtawajibika bila kutegeana,kwani ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha uhusiano alionao unakuwa na furaha wakati wote,haiwezekani katika muungano wa watu wawili kama mke na mume mmoja akaonekana kufaidi zaidi ya mwingine tupeane haki sawa kila mmoja amfurahishe mwenzie.

Inapendeza kuwa na amani na furaha kwa wote wawili kwani kila mmoja anajua jukumu lake kwa mwenzi wake ikiwa ni baba au mama alimradi kuwepo na maelewano baina yao,na kama utafahamu nini mwenzio anakipenda naye pia akawa anatambua kipi unapenda ni rahisi kudumu katika ndoa hata mahusiano kutokana na maelewano mazuri

Kama itatokea mahusiano yana mapungufu ya mmoja kukosa kujituma ili  kutimiza mahitaji ya ndoa kwasababu zilizo ndani ya uwezo,,basi uwezekano wa kuwepo na migogoro ni mkubwa,na katika hali kama hii haitashangaza suala la uaminifu kukosekana kutokana na kwamba mmoja anaona hapati mahitaji ya msingi kutoka kwa mwenzake mume au mke.maisha ya ndoa yanaitaji mawasiliano ya mara kwa mara,kwani kwa kufanya hivyo inaleta ushirikiano ,na uwazi ukiwa ni silaha ya kujenga zaidi..usinyamaze kimya kwa matatizo yanayojitokeza kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha mahusiano yenu.

Maoni 6 :

  1. heloooo
    nimefatilia mada..na imenigusa sana hasa kwangu..mimi niko ktk mahusiano...lakini....kuna upungufu wa mawasiliano na mwenzangu.. mtu anakwambia anakupenda but haonyeshi all that needed to be shown..to you..mfano hisia.. yaani hauoni hisia yeyote,.ya mapenzi,..and no care at all but ukiuliza wat is the problem anakwambia hamna..na anasema anakupenda...sielewi tatizo nini...na nashindwa....can you give some ideas

    JibuFuta
  2. Adela, nashukuru kwa hii mada, natumai na wewe sio mvuvi kwa mwenzako au?

    JibuFuta
  3. nashukuru tuko pamoja na pole sana ila inaonekana mwenzio ana matatizo kwani inakubidi ufanye uchunguzi zaidi kuna nini kinaendelea na hata wakati unapomuuliza akikujibu hakuna tatizo basi muelezee yote yanayokukwaza na kumuambia hayo ndiyo matatizo yake,vinginevyo kama ukiona habadiliki basi ujue ni muongo na ana lake jambo fanya uchunguzi wako kwa siri utagundua ukweli.kwani mtu anaweza akawa anakuambia anakupenda machoni kwasababu anakuonea huruma lakini moyoni hana lolote.

    JibuFuta
  4. @Emu three tuko pamoja yeah naamini mimi siyo.

    JibuFuta
  5. Mdada umenena.Mambo ya kutegeana big nooooooo.

    JibuFuta
  6. kweli dally ni vizuri kuwajibika ktk mahusiano ili kila mmoja aweze kutoa furaha kwa mwenzie kwani moja wapo ya sababu ya kuanzisha mahusiano ni kuitafuta furaha na faraja ya kweli

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.