Matunda ni mazuri sana katika afya ya binadamu,watu wengi hutumia matunda kabla ya kula chakula au baada ya kula chakula lakini kuna wengine huwa wanatumia matunda kama mlo wa mchana akiwa ameweka mchanganyiko wa matunda ya aina mbalimbali,na mtu huyu inawezekana anafanya hivi ikiwa nia ni kupungua uzito kwa kukwepa kula chakula ambacho kinaweza kumuongeza mwili kwa kasi, sizani kama kuna mtu asiyependa kula matunda ila inatokea baadhi wanachagua matunda wanayoyapenda, mtu asiyependa kabisa matunda basi atakuwa na matatizo.anahitaji ushauri kutoka kwa wataalamu kuhusu umuhimu wa matunda mwilini. |
Nakubaliana nawe matunda ni muhimu sana kwa afya na kwa kila binadamu. Na unaweza kula kila wakati Ahsante kwa kutukumbusha Adela. Ijumaa iwe njema kwako.
JibuFuta