Pages

Jumatatu, Oktoba 25, 2010

Watoto chini ya miaka 18 marufuku kushiriki katika harusi,,ni huko mkoa wa Kagera wilayani Karagwe.

 Watoto kama hawa ni baadhi ya watoto ambao wanashirikishwa katika usimamizi wa harusi mbalimbali na kujikuta wakiiga yale yanayofanyika katika harusi,Huko wilayani Karagwe Serikali imepiga marufuku kwa watoto chini ya umri wa miaka 18 kushiriki katika harusi kwani ni kichocheo cha kuongezeka kwa hisia za ngono kwa watoto,aidha pia imepiga marufuku watoto kuwa katika kumbi za starehe zaidi ya saa 12 jioni.


Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali(mstaafu) Fabian Massawe amesema hatua ya kupiga marufuku watoto kushirikishwa katika harusi inalenga kuwaweka mbali na matukio yanayoweza kuwajengea fikra za ukubwa kichwani mwao,amesema matukio kama watu wazima kulishana keki kwa kutumia ndimi na kubusiana mbele za watoto,kunaweza kuchangia watoto hao kuiga na kujiingiza katika matendo hayo,kabla hawajafikia umri stahiki.

Amesema wamepiga marufuku ikiwa ni pamoja na kuzingatia hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba watoto hupenda kuiga mambo wanayoyaona,amesema wamewaagiza maafisa watendaji wa vijiji, vitongoji na kata zote 24 zinazounda wilaya hiyo,kuhakikisha utekelezaji wa agizo hilo unazingatiwa.,,jamani watoto huwa wanatumiwa sana katika kusindikiza harusi na kufanya harusi  kupendeza zaidi sasa je mdau unasemaje kuhusu hilo la huko Kagera ipo sawa hiyo..

Maoni 5 :

  1. ha ha ha haaaaa! kaazi kwelikweli:-) watoto ni wazuri sana kwa kuiga na wanajifunza na kufanya majaribio kwa kila kitu wafanyacho wakubwa.....

    JibuFuta
  2. Hii kitu siielewi kabisa. Kwani watoto wanaoshiriki kwenye harusi kwa kuwa harusini watastukia wanaofunga ndoa watavuliana nguo baadaye?


    Kuna mambo mengine ni siasa za kipuuzi kwakuwa kirahisi ningedai kuwa watoto wanaoshiriki kwenye harusi wangeiga jambo zuri la kuoana na sio kuonjana tu nje ya ndoa.


    Ni mtazamo wangu tu.:-(

    JibuFuta
  3. Jamani hii sio haki kabisaaaaa,Je wale wanaoishi chumba kimoja baba mama na watoto na kuwaona wazazi wao wakifanya mambo ya kikubwa wafwanyweje? Wapigwe marufuku kuishi chumba kioja na wazazi wao?

    JibuFuta
  4. aina nyingine ya utumikishaji watoto kifikra/kiakili...child labor

    JibuFuta
  5. Huu wakati mwingine mimi nauita ubinafsi,ni ubinafsi wa kujijali wenyewe bila kujali maisha ya watoto hapo baadaye.
    Kama ukichunguza vizuri watoto hupenda sana kuiga, na huiga vile vyenye kuwaharibu. Na kwa hiyo kwa wazazi inabidi kuwa waangalifu sana.
    Kwenye ndoa, wanaharusi wanatakiwa wawe na uhuru, na kwao wao tukuchukulie hawajabahatika kuwa na `watoto' kwahiyo hawajui kuwa kwenye hadhira kuna watoto ambao kwa matendo yao wataiga...sasa kwanini tuwalete watoto harusini, na kuwanyima uhuru `wakubwa' kujimwaga!
    Sijui mimi naona wazo hili ni zuri! Tujaribu kuwaangalia maisha yao ya baadaye na mambo yao yaendane na umri wao...sijui ni wazo na mimi
    Ni kweli mkuu huu ni utumikishwaji kwa watoto ki-akili...wanakomazwa!

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.