Pages

Jumanne, Novemba 30, 2010

Msimu huu wa matunda tuzingatie usafi



Kipindi hiki ukipita katika maeneo mbalimbali ya jiji utagundua kuwa msimu wa matunda umeanza hasa maembe na mananasi,kwa harakaharaka wengi wetu hutumia msimu huu kwa ajili ya kujenga afya zetu,lakini mbali na ujenzi wa afya kuna kipindi ambacho wauzaji wa matunda hayo hujisahau na kuanza kuyauza katika mazingira machafu,hivyo kuchangia kuzibomoa tena afya zetu badala ya kuzijenga.

tukumbuke kuthamini usafi katika mazingira ya kutayarisha matunda hayo kwani kuna maradhi ya aina mbalimbali kama utashindwa kuzingatia usafi kama kipindupindu,kuhara na matumbo na hata kusababisha vifo

Msisitizo usafi binafsi kuanzia katika makazi yetu  tunayoishi kila siku, pia kuosha matunda kabla ya kula,na baada ya kula ni jambo la muhimu kula matunda katika hali ya usafi ili kujenga afya na si kuibomoa afya.

Maoni 1 :

Unakaribishwa kutoa maoni yako.