Pages

Jumatatu, Novemba 29, 2010

Wanandoa wa jinsia moja kukamatwa huko Kenya .

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga pichani ameagiza kukamatwa maramoja wanandoa wa jinsia moja  kwa kile alichodai  kuwa tabia hiyo siyo ya kimaadili,Odinga ameyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kamukunji vilivyopo katika jimbo lake la Langata ambapo amesema kuwa tabia hiyo siyo ya asili ya Wakenya. "endapo mtawabaini wanandoa wa jinsia moja ni lazima wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya mamlaka husika" alisema Waziri Mkuu Odinga.

Hawa ni miongoni mwa wanandoa wa jinsia moja.pia alisema ni kitendo cha uendawazimu mwanamume kuangukia katika mapenzi na mwanamume mwenzake wakati kuna idadi ya kutosha ya wanawake ambapo sikuzote wanawake ni wengi kuliko wanaume.

Jamaa wakifurahia ndoa yao,,Taarifa ya Odinga inaweza ikakwaza jitihada za wanaharakati ambao hivi karibuni waliamua kujitosa katika kampeni za kupinga ubaguzi dhidi ya wanandoa ya jinsia moja..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.