Pages

Jumapili, Desemba 05, 2010

Swali kutoka kwa Mary limenijia leo nikiwa KAZINI,," nina mimba ya bosi wangu lakini mama mwenye nyumba hajui,,nafsi inanisuta nataka niseme ukweli"

Kuwa na mimba ni jambo la kawaida kwa mwanamke lakini inabidi kuwa makini sana kama haujajipanga,, Kuna msichana anaitwa Mary ana miaka 21 ni msichana wa kazi za ndani mkoani Dar  es salaam alikuja studio leo akawa anaomba ushauri kuwa amepata ujauzito wa bosi wake ambaye alikuwa akimlazimisha kuwa naye kimapenzi wakati mama mwenye nyumba akiwa hayupo,,sasa Mzee amemuambia amdanganye mama mwenye nyumba kuwa mimba ni ya mtu mwingine ,Mary anasema akafanya hivyo na kumuambia yule mama kuwa mimba ni ya mtu mwingine na aliyempa mimba amemkimbia na huyo mama mwenye nyumba kutokana na huruma akamwambia Mary aendelee kukaa atamsaidia,,lakini Mary anasema siku zinavyozidi akimuona yule mama roho inamuuma anataka amwambie ukweli kuwa ile mimba ni ya mume wake,,na anajuta sana kwa yote yaliyotokea,,Je unamshauri nini kwa hili........

Maoni 4 :

  1. KWANZA NAMPA POLE SANA MARRY KWA TUKIO HILO.PIA AJITAHIDI KUWA MVUMILIVU ILI APATE NAFASI YA KUILEA MIMBA YAKE PAMOJA NA MTOTO ATAKAYE ZALIWA BILA MATATIZO HUKU AKIJUA KILE ANACHOKIFANYA KWANI AKIFUNGUA KINYWA AKASEMA ATAKOSA HATA HUO MSAADA.KILA BINADAMU ANA UELEWA TOFAUTI INAWEZEKANA AKAFUKUZWA NA HATA HUYO MWENYE MIMBA ASIMUONE KABISA.CATHERINE P. MYAKA.

    JibuFuta
  2. Alikulazimisha, hii naiona haijakaa sawa, labda ungesema alikubaka! Vyovyote iwavyo, swali kubwa la kujiuliza ni je `kama ni mimi nimefanyiwa hivyo ingekuwaje', uchukulie wewe ni mama mwenye nyumba imetokea hivyo kwa mfanyakazi wako na mumeo ungejisikiaje?
    Hali livyo, lazima ipo siku ukweli utadhihiri, cha msingi ni mawili, umwambie baba amwambie mwenyewe mkewe, au wewe umwambie mama mwenye nyumba! Kwani akigundua badaye atajua kuwa wewe na mumewe mlikuwa na mahusiono, ndio maana mambo hayo yameenda kisirisiri.
    ONYO: Kama ukilazimishwa na baba mwenye nyumba, haraka mwambie mama mwenye nyumba, kabla haijafika pabaya, na kama ni kubakwa, sheria itachukua mkondo wake! Tatizo ni kuwa `mnapenda iwe hivyo'! Ndio maana mnatongozwa mnakubali, mkisingizia kuwa `mumelazimishwa...' kweli unaweza kulazimishwa kwa kuambiwa usipokubali utafukuzwa, kazi, ...ikiwa ni hivyo ongea na mama mwenye nyumba, muweke mtego, ili kabla, mchi haujadunda kwenye kinu, mama ajitokeze, na hapo baba ataumbuka na itakuwa mwisho wa kukusololea.
    Ni wazo tu bibiye
    Kiukweli tendo hilo linauma sana kufanyiwa,

    JibuFuta
  3. Amshataki huyo Baba kwa kumpa mimba, nahisi aliji force kwa huyo binti.
    Pole sana Binti that is awful ni unyama wa huyo baba asipo sema wazi atarudia kwa mtu mwingine.

    JibuFuta
  4. Hakuna kulazimishwa wala kubakwa hapa tusidanganyane, siku hizi suala la ngono kwa vijana linakuwa la mapema mno kiasi kwamba binti mdogo kutembea na baba aliyemzidi umri kama vile si tishio tena.
    Kuna jambo halijaenda sawa hapo kwenye mahusiano labda baba anakataa kutimiza ahadi fulani fulani walizoahidiana ndio maana binti anaamua kutoa taarifa. Vinginevyo mpaka mimba inaingia si uhusiano wa siku moja ni wa muda ulikuwa siri ya wawili hao.

    Ushauri akina mama acheni kuwaachia huduma za karibu wasichana wa kazi kwa waume zenu, mwanaume ni kama mbuzi ukimpitisha karibu na majani bila kumvuta kwa kamba hataacha kula majani hayo!

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.