Ijumaa, Desemba 03, 2010

Usafi wa jikoni katika nyumba yako ni wa muhimu kufanyika mara kwa mara na uwe wa kudumu.

Haipendezi kukuta mazingira ya jiko yapo kama hivi safisha mazingira ya jikoni mwako mara kwa mara na uwe ni wa kudumu, kwani kama unapika chakula katika mazingira machafu basi utakuwa unalisha familia yako chakula ambacho sio kisafi

Ni muhimu kupanga vifaa vya jikoni kila kifaa mahali pake kama ni kabatini basi uviweke na sio kuweka kila mahala mara mezani mara kabatini haipendezi.,safisha vifaa vyako vya jikoni kausha vizuri na uhifadhi katika hali ya usafi.

Inapendeza kuona mazingira ya jikoni yakiwa katika hali ya usafi kama hivi na haijalishi jiko lako ni la kifahari au sio la kifahari ni lazima liwe katika mazingira ya usafi wakati wote,epuka kulaza vyombo vichafu jikoni,safisha sakafu ya jiko na sehemu zilizojificha kama ndani ya kabati nk.hakikisha unapomwaga kwa bahati mbaya chai,chakula au kinywaji chochote katika meza ya jikoni unafuta mara moja na kuiacha meza yako ikiwa safi


HABARI NDIO HIYO JIKO LIKIWA SAFI INAPENDEZA   KUPIKA CHAKULA KINAKUWA KATIKA HALI YA USAFI.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom