KITABU MALIPO NI HAPA HAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA ..... Jamal alilia sana, huku akimkumbuka marehemu mama yake. Hata hivyo aliamua kumwomba msamaha baba yake pamoja na mama yake mdogo, halafu akaelekea chumbani.
“Laiti mama angekuwepo haya yote yasingetokea, yaani baba ananipiga kwa sababu ya huyu mwanamke inaniuma sana.” Aliwaza Jamal na kuhuzunika sana.nini kinaendelea usikose sura ya 11.......
INAPOENDELEA...Kadiri
siku zilivyozidi kwenda mama mdogo alizidisha visa na kuanza kumsingizia
mambo ya uongo kwa baba yake. Kutokana na kusingiziwa na mama
mdogo Jamal alikuwa akipigwa sana kila wakati hali iliyomkatisha tamaa
Jamal. Jamal alitamani kutoroka lakini alivumilaia kwani alikumbuka
maneno ya
mama yake mzazi alivyokuwa akimwambia kuwa zile mali ni zake
pamoja na mdogo wake Aisha. Hivyo ilimbidi aendelee kuishi katika hali ya
mateso.
Hatimaye
matokeo ya Kidato cha Nne yalitoka na kwa bahati mbaya Jamal hakufaulu
vizuri katika mitihani yake, kwani alipata daraja la tatu (division three).
Hata hivyo kulikuwa na uwezekano wa kusoma shule
binafsi. Kufuatia
matokeo hayo Jamal alilia sana kwa uchungu kwani hata baba yake
alimgombeza sana baada ya kuona kuwa amefeli ingawa mwanzoni aliahidi
kumtafutia shule binafsi ili kuendelea na Kidato cha Tano.
Siku moja
Jamal alikuwa amekaa chumbani kwake akijisomea kijitabu kimoja cha
riwaya kiitwacho “Shija“. Ghafla aliingia mama yake mdogo na kuanza
kumsemesha kama kawaida yake.
“Jamal
mbona unanitesa hivi lakini? Ina maana hunielewi au hutaki kunielewa?”
Aliuliza mama mdogo huku akikaa kwenye kitanda cha Jamal.
“Nilishakwambia
siwezi kuwa na wewe. Kwanza najua wewe ndiye chanzo cha baba
kunipiga bila sababu. Pili, kwa mila na desturi baba na mtoto wake
hawawezi kuchangia mwanamke. Tatu sikupendi. Nne wewe ni Malaya.
Tano unataka kuniharibia maisha yangu. Ila yote haya yataisha kwani
karibia nakwenda zangu shule.” Aliongea Jamal kwa mama yake
mdogo huku
akirusha mikono kama anasoma ngonjera.
“Unajiona
mjanja, baba yako atakupeleka shule nikiamua hata hiyo shule huendi.”
Alijibu mama mdogo huku akicheka kwa dharau. “Inamaana
mama mdogo yote unayonifanyia unaona haitoshi na sasa unataka
hata kunizuia nisiende shuleni? Nakwambia shuleni nitakwenda na huwezi
kupinga hata kidogo.” Aliongea Jamal kwa kujiamini. “Tutaona
nani mjanja.”Alisema mama yake mdogo na kubamiza mlango
na
kuondoka.
Baada ya
siku tano kupita tangia mama mdogo na Jamal wajibizane maneno ya kukashifiana,
mama mdogo alifikiria na kubuni njia nyingine ya
kumfanyia visa Jamal.
“Sasa hebu
nibuni kisa ambacho baba yake akisikia tu hata nia ya kumpeleka
shule Jamal itakufa. Mwanamke siku zote ni mjanja kupita mwanamume.
Na mbinu hii ni komesha.” Aliwaza mama mdogo.
“Nitamtafuta
mwanamke na kumweleza yote kuhusu ninavyompenda Jamal, na
jinsi kijana huyu anavyonisumbua. Kisha nitamwomba aniandikie
ujumbe wa uongo utakaoonyesha Jamal ameandikiwa na mwanamke,
halafu nitampa baba yake ili akiusoma asimpeleke shule. Nafikiri
hapo nitakuwa nimempata.” Aliwaza mama mdogo.
Baada ya
kupata hilo wazo mama mdogo alifanya hivyo na kisha kumpelekea
ile barua baba yake na Jamal. Siku hiyo baba Jamal aliwahi kurudi
nyumbani na kumkuta mke wake amekaa sebuleni akimsubiri. Jamal yeye
alikuwa amekaa chumbani kwake.
“Mume
wangu hii bahasha ndani ina ujumbe kuna msichana ameiletanimpe
Jamal nimefungua nikasoma niliyokutana nayo nimeshindwa kuamini
macho na akili yangu nimeona nikupe kwanza uisome uone mambo
anayofanya mtoto wako.” JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA 12
mhhhhhhhh htr ila unatutendaje sasa?mna kila ck tunafungua hkn kitu.
JibuFutawe ma mdogo una tabia mbaya sikupndiiii
JibuFutaHabari Debby, naifurahia kazi zako big up kweli wanawake tunaweza without kuwezeshwa, sina comment kuhusu kinachoendelea hapo juu ila nia yangu ni kujua kabila ambalo mwanamke anatakiwa kutembea na shemeji zake zote according to your program uliyoirusha passion radio pliiiiiiz naomba uniambie.
JibuFuta