Pages

Alhamisi, Septemba 20, 2012

" NAMPENDA SANA LAKINI AMEAMUA TUACHANE KWASABABU MAMA MKWE ANITAKI NIFANYEJE JAMANI NAOMBENI USHAURI" ANAOMBA USHAURI WENU WADAU KUPITIA BLOG YA ADELA


Hello dada adela,habari!!,leo nimetembelea blog yako na nimeipenda sana, hapa leo nimekuja ili kuomba ushauri dada yangu,mi ni msichana wa miaka 25,miaka 5 iliyopita nilipata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi fulani, niliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na kaka mmoja tulikuwa tunasomanaye chuo kimoja,he is from kenya.tuliendelea na mapenzi yetu mpaka tukamaliza shule,na akaniambia kuwa anataka kufika mbali na mimi(kunioa)basi tukarudi nyumbani.

yeye kwao(kenya)na mi kwetu (Tanzania).mwenzangu akapata kazi,sasa akawa anataka kuja kujitamblisha kwetu,akawa ameongea na mama yake,but tatizo ndio likaanza hapo,mama yake hataki kabisa kusikia,hataki mwanae aoe mtu wa taifa lingine zaidi ya mkenya.akajaribu kuongea na mama yake tena lakini wapi akakataa,mpaka mama yake akamnunia mwanaye basi  ilibidi mpenzi wangu anieleze,yaani niliumia sana
nae akawa anaumia sana.

ilibidi  tuendelee hivyo tukiwa na hope labda mama yake atabadilika,baada ya miezi kama kumi,akamwambia tena mamayake lakini bado anakataa anasema hataki kusikia yeye hatampa baraka zozote,hii ilikuwa mwezi uliopita.sasa mpenzi wangu anasema basi tuachane,kwani anaogopa kutokuwa na maelewano na mamayake.kwani ndie alimlea peke yake,bila baba yao ataki kumchukiza mama yake,sasa mi bado nampenda sana huyu kaka na yeye bado ananipenda lakini hilo ndio tatizo,naona siwezi kumuacha,na mama mkwe ndio tatizo sijui nifanye nini?



Maoni 7 :

  1. Pole sana mpedwa,usilazimishe,muombe mungu atakupa wakufanana na wewe.maana kama huyo mwanaume amesha sema hivyo huna jinsi.pole sana.

    JibuFuta
  2. Pole sana mpedwa,usilazimishe,muombe mungu atakupa wakufanana na wewe.maana kama huyo mwanaume amesha sema hivyo huna jinsi.pole sana.

    JibuFuta
  3. pole dada kwakweli hiyo ni ngumu kumeza wewe umesahau ya kuwa wakenya wanaukabila hata wao wenyewe kwa wenyewe hakufaa rangi itakuwa chokaa? ninamaana wakenya kwa wakenya tu hawaowani wanaowana kabila kwa kabila ss itakuwa wewe wa nchi nyingine pole dada hiyo hakuwa bahati yako omba Mungu akupe wako kwako ambaye atakupenda na wewe utampenda pasipo kuwepo vikwazo pole sana usijali hayo ndio maisha

    JibuFuta
  4. Hi dia.Pole kwayaliyokusibu. Ila ukiona kitu kama hicho kimetokea kabla ya kufunga ndoa shukuru mungu.Mimi ni mama mwenye watoto watatu,kabla yakuolewa na kufunga ndoa nilikuwa namahusiano ambayo kwa macho ya kibinadamu nilikuwanikidhani ndo mume. Na hata ilipotokea tuka achana moyo uliteseka sana baadae nikazoea na hatimae nikapata mume kutoka kwa mungu. Hadi sasa navyoandika hivi yule niliyedhani ni mchumba alishaoa kama mala mbili nakuacha. Nachotaka kusema ujalibiwapo usitende dhambi, na kila jaribu linamlango wa kutokea.Omba mungu akupe mume wako na amini yupo,maandiko yanasema mume mwema hutoka kwa mungu. Kama huyo kijana ni wako hata wazazi wake wakatae itafika mahali atakuwa wako tuu. Maisha ya ndoa ni ya watu wawili na ndoa sio girl friend na boyfriend inaitajika awe wa ubavu wako vinginevyo mtaachana. Mungu akubariki na akuonyeshe ubavu wako. uwe na amani mdogo wangu.

    JibuFuta
  5. Kwa kweli mapenzi ya kiafrika ni tofauti sana na yale ya kizungu...kwa wenzetu mapenzi ni ya wawili zaidi..ndio maana waweza kukuta hata wakaenda kufunga ndoa wakiwa wawili tu na wapambe wao na baada ya hapo wakatokomea ka honeymoon. Hata familia zao ni veeery nuclious; baba, mama, watoto na possibly some pets kama mbwa na paka. Kwetu ni ngumuu...mapenzi ya wawili ni kabla hamjaoana. Mapenzi ya ndoa yanaunganisha familia. Hivyo ni jambo jema kuangalia pia mtazamo na misimamo ya familia katika mahusiano yako na mtarajiwa wako. Kama utakua kichwa ngumu, waweza kukosana na ndugu, kukosa baraka na hatimaye kukosa furaha ya maisha kabisaaa. Hata hivyo, kama kijana ataonesha msimamo thabiti na kumtaka mama yake aseme ukweli ulio dhahiri sababu halisi ya kukataa yeye asioe mtu wa taifa jingine ni nini, inakua nzuri zaidi. Mwaweza pia kutumia ndugu walio na mawazo mbadala na misimamo ya wastani wakawasaidia kubadili mawazo ya mama. Waweza kukuta mama ana mifano ya ndugu waliooa jamaa wa mataifa mengine na mwisho wao haukua mzuri na hvyo mama akaaminishwa kua tatizo lisingekuwapo kama wangeoana watu wa jamii na kabila moja. Hata hivyo, mkiwa na mapenzi ya dhati kabisa, wewe na mwenzio na ndugu na jamaa wakajua hilo, lazima mtapata sapoti ya kutosha na mama akibaki peke yake katika msimamo huo, basi itakua ni rahisi kubadili uamuzi wake. Ila kama hata mapenzi yenu watu wana mashaka nayo!!! hapo ni sooo

    JibuFuta
  6. Inawezekana unadanganywa na huyo mpenzi wako.Hayo unayolishwa kutoka kwa mkwe mtarajiwa inawezekana siyo hivyo tatizo labda ni huyo mpenzi wako ana mwanamke mwingine. Labda kama angekupewleka kwao na huyo mama yake akakukatae live au ukajionee jinsi atakavyokupokea ndipo utagundua kama kweli huyo mama anakukataa. Usiridhike na maelezo ya huyo kwa sababu wewe unampenda.Kina dada inaelekea hamuwafahamu wanaume vizuri ninyi ndio maana mnazidi kuumizwa kwa kusema nampenda, nampenda x7x70. Huwa hamna nafasi ya kukaa kutafakari juu ya maisha yenu na mafanikio yenu na nafasi mlionayo katika jamii na maisha ya mbele. Huwa mnadanganywa kirahisi mno (Siyo wote.yAANI UNAWEZA KUONA TU JINSI MTU ASIVYOWAZA MBALI ZAIDI NA KUGANDA MAHALI PAMOJA BILA KUFUNUA MFUNIKO ULIOFUNIKA LILILO MBELE YAKE.Jaribuni kuwa watu wa kujiamini sana na kujitambua. Tena mbaya zaidi kwa kuwa amekulala na kukuvua chupi basi hapo kishakuloga na hutaki kutoka hapo.

    JibuFuta
  7. asanteni kwa ushauri wadau-MTAKA USHAURI

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.