Pages

Jumatano, Oktoba 17, 2012

Je ni sahihi mwanamke kumsachi mwenza wake ili kujua kiasi cha pesa aliyonayo.

kuna baadhi ya wanawake wanayotabia ya kuwasachi wenza wao pale ambapo akimuomba hela  akiambiwa sina pesa basi anaanza kumsachi ili kuangalia kama kweli anayo pesa au la, au wakati mwingine hata kabla ya salamu moja kwa moja unakimbilia kwenye mfuko wa shati au wa suruali na kutaka kujua kiasi cha pesa aliyonayo,Baadhi ya wanaume wameilalamikia tabia hiyo kutokana na namna mwanamke anavyompekuwa na kutaka kujua ana pesa kiasi gani, hususani ambao hawajafunga ndoa JE WEWE UNASEMAJE KWA WALIO KWENYE NDOA INAWEZA KUWA NI POA  AU NI KERO..........

Maoni 1 :

  1. Mapenzi ya pesa, mapenzi ya kutokuaminiana ndivyo yalivyo, hata wakati mwingine najiuliza kwanini pia mke na mume hamchangii simu. Kila mmoja hataki mwwenzake aguse simu ya mwenzake.

    Mkioana mnakuwa kitu kimoja, sasa mnapoanza kuwekeana mipaka, mnaibomoa ndoa yenu kwa mikono yenu wenyewe.

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.