Binafsi ninapokuwa na matatizo au hasira ya jambo fulani huwa naona ni vyema nikilia baada ya hapo huwa najisikia kama napata ahueni ya kile nilichokuwa nakiwaza ni kweli kuna baadhi ya watu ambao huwa hawana machozi ya karibu kiasi kwamba hata kama amepatwa na matatizo huwa anaumia tu moyoni lakini haonyeshi kulia na katika hili inasemekana wanaume wanaongoza kwa kuumia moyoni kwani wenyewe huwa ni vigumu kutoa machozi wataalamu wanakuambia unapotoa machozi unapunguza maumivu kama unajisikia kulia kutokana na tatizo lolote ulilonalo basi yaachie machozi yatoke na baadaye utaona utakuwa sawa na kuendelea kutafakari changamoto zote . |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.