MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOLEWA BURE
Taasisi Isiyokuwa ya Kiserikali ya Rafiki Elimu FOUNDATION kupitia Mradi wake ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI inapenda kuwatangazia vijana wote wa kitanzania wenye umri wa kati ya miaka kumi na tano ( 15 ) hadi Arobaini na Tano ( 45 ) nafasi za kushiriki katika mafunzo ya ujasiriamali.
Mafunzo yatakayo tolewa ni pamoja na :
i Utengenezaji na Uzalishaji wa Bidhaa za aina mbalimbali kama vile :
a. sabuni za aina zote
b. batiki
c. chaki za aina zote.
d. Mishumaa.
e. usindikaji wa vyakula, vinywaji& matunda
f. Uokaji wa mikate,
g. utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama vile mikanda na viatu kwa kutumia ngozi za wanyama zilizo sindikwa.
h. Utengenezaji wa viungo vya vyakula vya binadamu kama vile Chilli Sauce, Tomato Sauce, Mango Picco , Peanut Butter nakadhalika.
i. Utengenezaji wa mkaa kwa kutumia makaratasi.
j. Utengenezaji wa kiwi.
k. Utengenezaji Wa Vyakula Vya Mifugo kama vile kuku na n’gombe.
l. Mbinu Za Ufuaji Bora.
II . Mbinu za kilimo Bora.
ii. Elimu Ya Ujasiriamali.
iii. Elimu Ya Sheria Za Biashara.
iv. Elimu Ya Usimamizi na Uongozi Wa Biashara.
v. Ubunifu, Uendeshaji na Usimamizi Wa Miradi
vi. Uandishi Wa Miradi Mbalimbali.
vii. Elimu Ya Uwekaji na Ukopaji Fedha .
viii. Elimu Ya Uendeshaji wa Vikundi Vidogo Vidogo Vya Kuweka na kukopa Fedha.
ix. Elimu Ya Utengenezaji na Utafuta wa Masoko.
ADA YA USAJILI : Ada ya kujisajili katika mradi huu ni BURE.
ADA YA MAFUNZO : Ada ya kushiriki katika mafunzo haya ni BURE.
MWISHO WA KUJIANDIKISHA : Tarehe 25 OKTOBA 2012.
KUANZA KWA MAFUNZO : Tarehe 01 NOVEMBA 2012.
KUZINDULIWA KWA MRADI : Tarehe 23 OKTOBA 2012.
NAMNA YA KUJIANDIKISHA : Fika katika ofisi zetu zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
Panda gari za UBUNGO - CHANGANYIKENI, kisha shuka kituo kinaitwa TAKWIMU. Ukifika TAKWIMU fuata barabara ya lami hatua ishirini ( 20 ) kisha tazama upande wako wa kulia utaona bango la ofisi yetu limeandikwa RAFIKI ELIMU FOUNDATION.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu
0763976548 AU 0782405936.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Mradi Huu, tembelea blogu yetu : www.rafikielimu.blogspot.com
HABARI NZURI HIZO MPENDWA,TUPO PAMOJA
JibuFuta