Pages

Jumatano, Oktoba 31, 2012

UVAAJI WA BANGILI HUONGEZA MVUTO ZAIDI


Bangili ni kitu kilichotengenezwa kwa ajili ya kuvaliwa mkononi n akuongeza mvuto kwa mrembo  zipo aina mbalimbali za bangili za utamaduni ambazo zinatumia shanga za kimasai zingine hutumia madini kama dhahabu na nyinginezo 

Bangili unayotaka kuvaa inategemea na nguo ambazo unataka kuvaa kwani kuna wale ambao wanapenda  kuvaa bangili zilizotengenezwa kwa malighafi kwaajili ya kuendana  wengine hupendelea bangili zilizotengenezwa na vitu vya asili kama vifuu vya nazi inaaminika bangili zilizotengenezwa na vifuu vya nazi zimekuwa zikipendeza kuvaliwa kutokana na muonekano wake  na gharama yake ni nafuu 

uvaaji wa bangili pia unatakiwa kuzingatia rangi ya mvaaji kama mtu ni mweusi anashauriwa kuvaa bangili zenye mng'ao ili kuweza kuwa na muonekano mzuri zaidi 



Ni vyema kama utazingatia mpangilio wa rangi katika uvaaji wa bangili na itapendeza kama uvaaji huo utazingatia nguo uliyovaa, viatu au mkoba na hereni. 

Maoni 1 :

  1. Mambo ya urembo hayo, yapo ya kila aina, bangili, ushanga,kidani,na sijui nini tena, ....Tupo pamoja mpendwa

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.