“Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani mwaka huu yanabeba ujumbe ule ule uliotolewa mwaka jana ambapo kauli mbiu hii inaendelea mpaka mwaka 2015 na kwa mwaka huu jijini Dar es salaam yanafanyika katika uwanja wa Biafra yakiongozwa na kauli mbiu ya Tanzania Bila Maambukizi Mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana”
lengo la kauli mbiu hiyo ni kuhamasisha na kuelimisha zaidi jamii kuhusu VVU na Ukimwi na kubadilisha tabia ili kujikinga na maambukizi haya mapya ya VVU, kuhamasisha jamii kuacha kabisa unyanyapaa, unyanyasaji na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU, na kuboresha huduma za afya na tiba ya magonjwa nyemelezi na dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs).
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.