Pages

Jumatatu, Machi 18, 2013

JE UNAFIKIRI MPENZI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII KAMA FACEBOOK NA TWITTER ANAWEZA KUWA MUME AMA MKE BORA?????

Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada, sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia mitandao ya kijamii kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka kuanzisha  kwani unahitaji kumfahamu zaidi  na ndipo utakapoweza kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.

Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na maamuzi yako.

Maoni 1 :

  1. Inaweza `Ikawa', CHANZO, kwani mwisho wa siku ni lazima mkutane, mkubaliane, mjuane, sizani kama itaishia ndani ya uso wa kitabu na mkafikia kusema `nataka uwe mchumba, rafiki au kuwa mke na mume wangu'...

    Mitandao kama sehemu nyingine ya mawasiliano, ni kama `kutangaza' humo kwenye mitandao ni kujuana kwa kuwasiliana, bado kujuana kwa undani zaidi,...ambayo ndio muhimu.

    Kuna lugha ya mitandao, haiwezi kukidhi haja, ....lugha hiyo inaweza ya ikawa ya kudanganyana tu.

    Inaweza ikatokea , mkakutana ambao kweli mna nia njema, na kweli mkapatana, na ikawa ndio `njia ya kujenga urafiki', ....imeshatokea, na watu wametoa ushuhuda.

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.