Mimi
naitwa George naishi Iringa nampenda mwanamke mmoja aitwa Happy nimekaa
na happy kwa muda mrefu bila kumuambia nampenda nimejitolea kwa kila kitu
wakati akiwa shule kamaliza shule bado nikawa nafanya kila kitu
kwaajili yake mwishowe nikamwambia ukweli kuwa nampenda ila alinikataa
akaniambia yuko na mtu anayempenda sana, Jamani naumia nisaidieni
nampenda kwa muda mrefu Sana sijawahi kupenda hivi na nikimuita popote
pale tuonane hakatai na huwa ananinunulia hata zawadi wakati mwingine
ila kuwa na Mimi kimapenzi hataki, ijapokuwa mimi nimejitolea kwake kwa kila kitu nimeshamsaidia sana katika maisha yake. Nakosa raha sana, nampenda sana Happy sijui nifanyeje Jamani.
George elewa kuwa Happy sio chaguo lako tayari anaye anayempenda kwa moyo wake wote.
JibuFutanilichojifunza hapa ni kwamba Happy alikufanya rafiki kama rafiki zake wengine (wakike) ndo maana hakusita kuandamana na wewe popote, akakupa zawadi lakini hakuwa tayari kuwa nawe kimapenzi, hili ni jambo la kawaida kwa binadamu waweza mpenda mtu awe rafikiyo wa kusaidiana hapa na pale, kubadilishana mawazo na mambo mengine mengi lakini kamwe usitamani awe mwandani wako.
NAKUBALIANA NA ULE USEMI USEMAO URAFIKI UZAA UCHUMBA LKN SI KILA URAFIKI HUFIKIA HATUA YA UCHUMBA. HEBU JARIBU KUBADILI MSIMAMO NA ULIKUBALI HILO NA KAMWE USIMUHUKUMU HAPPY KWA MAAMUZI NA MSIMAMO WAKE