Jana ni siku ambayo Daimond aliweza kukamilisha ahadi yake ya kuwaandikisha shule watoto walioweza kucheza Ngololo kupitia blog yake ya wasafi.blogspot.com Daimond amesema
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa fursa
ya kuiona siku nyingine nikiwa na Afya njema
kabisa,ilikuwa ni
siku niliyopanga kutimiza ahadi yangu ya Kuwapeleka shule watoto
walioshinda shindano la kucheza ngololo.. na kwa vile nilitaka wapate elimu iliyo bora
zaidi,nilikaa na management yangu..na
kutafiti ni shule ipi itakayokidhi mahitaji ya watoto wale,shule yenye
mazingira mazuri
ya kusomea
na yenye standard nzuri. sote tulikubaliana kuwapeleka shule ya
EAST AFRICA INTERNATION SCHOOL,iliyopo Mikocheni. napenda kumshukuru mkuu wa shule hii,Bi Mercy
Githirua kwa kutupokea vizuri mimi na
watoto wale..lakini pia kuwashukuru wanafunzi wote kwa kutupokea vizuri
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.