Wakati mwingine mtu unaweza kuona kitu fulani, lakini ukawa unajiuliza "Hivi pale patakuwa na kitu gani au kile ni nini?" Na huku ukiwa unajiuliza na kukosa majibu, lakini unaambiwa siyo kila kitu unatakifahamu wewe mwenyewe, ni vyema angalau ukauliza ili uweze kuambiwa ni kitu gani kile unachokiona. Ni sawa sawa na kusikia jambo fulani limetokea, na haraka haraka mtu anachukua na kusambaza habari kwa watu wengine, bila kuwa na uhakika kama kile kitu kina ukweli ndani yake.
Kwa mfano Mwanaume ameambiwa mke wake anatoka nje ya ndoa, moja kwa moja bila ya kufanya uchunguzi akaamua kumfukuza mke wake halafu baada ya siku mbili tatu unagundua yale yalikuwa ni maneno ya uzushi ,Ni bora kuchunguza kwanza kuliko kuchukua maamuzi ya haraka. SIKU ZOTE HARAKA HARAKA HAINA BARAKA |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.