HII NI SIMULIZI YA PILI KATIKA KITABU HIKI KILICHO NA SIMULIZI TATU TOFAUTI ENDELEA KUPATA UHONDO
ILIPOISHIA“Kumbe wewe ni shemeji yangu?” Ilikuwa ni sauti ya Eliza mdogo wake
Upendo ambaye aliwafanya watu wamshangae ana matatizo gani. Ndipo
kabla hajaendelea kuzungumza alianguka na kuzimia.
Wazazi wake walishangaa nini kimetokea na huyo Juliasi ni nani.
“Kuna nini jamani mwanangu amekuwaje leo?” Aliuliza mama Upendo
huku akionyesha mshtuko mkubwa. Basi ndugu walimchukua na
kumpeleka ndani huku akipepewa.
USIKOSE MWISHO WAKEINAPOENDELEA
Upendo alishindwa kuelewa kwa nini mdogo wake alitamka maneno yale,
basi alimshika James mkono.
“Mmh! Mdogo wangu atakuwa na matatizo makubwa sijui ana nini hebu
twende ndani tukamwone.” Alitamka Upendo huku wakiondoka kuelekea
ndani.
Wakati huo wote James alikuwa kimya kijasho chembamba kikimtoka kwa
kuogopa kilichotokea hivyo alishindwa kuongea chochote zaidi ya
kumfuata Upendo.
Walipoingia ndani walimkuta Eliza ameshazinduka. Alipomwona tu
James alisimama na kumshika kwa nguvu huku akilia kwa sauti ya juu.
“Kwa nini unafanya hivi? Unataka kutuangamiza mimi na dada yangu
Juliasi? Mimi nilikupenda sana na tayari nina mimba yako. Loh! Kumbe
ulikuwa una mwanamke tena dada yangu?” Aliongea Eliza kwa hasira na
hisia za ajabu huku Upendo akibaki anashangaa na kuuliza.
“Vipi Eliza mdogo wangu umechanganyikiwa? Huyu ni James sio Juliasi!”
Upendo alijaribu kumfariji mdogo wake.
“Sijachanganyikiwa dada yangu huyu bwana nilikutana naye Arusha
akaniambia kuwa anaitwa Juliasi. Naomba mmuulize mwenyewe aseme
ukweli.” Alisema Eliza kwa uchungu huku wazazi wake wakiwa hawaelewi
kinachoendelea.
Je, ni kweli anayosema Eliza?” Upendo aliuliza huku alimwangalia
James.
James alikaa kimya kwa muda kisha alikaa chini kwenye kochi huku
akiwa
ameinimisha kichwa chini kwa aibu na fedheha.
“Upendo yote aliyosema Esta ni kweli, naomba unisamehe ilikuwa ni
bahati mbaya sikujua kama ingekuwa hivi. Nisamehe mpenzi wangu
nilimfahamu Eliza kwa jina la Esta, siwezi kukupoteza nisamehe
mpenzi.”
James aliomba na kukiri mbele ya wazazi wake Upendo na wazazi na
ndugu zake. James aliyasema hayo akiwa bado ameinama chini huku
machozi yakimlengalenga kwa aibu na hofu ya kumkosa Upendo.
“Hivi ninasikia au naota jamani, wewe James leo hii unanifanyia hivi?
aibu
gani hii jamani? Angalia sasa umempa mimba mdogo wangu na mimi nina
mimba yako tayari hivi nifanyeje? James Mimi siwezi kukusamehe.”
Upendo aliongea kwa jazba huku amemkaba James shingoni kisha
akamwachia na kukimbilia nje.
Watu walimfuata ili kumshika lakini aliwazidi mbio na kutokomea
gizani.
Sherehe ilivunjika, watu wote wakatawanyika kumtafuta Upendo. Upendo
alikimbia kwa mbio za ajabu kama mbwa mwenye kichaa, hakujali kabisa
kiumbe alichokuwa nacho tumboni. Wakati watu wanaanza kumtafuta
Upendo tayari alikuwa ameshafika mtaa wa tatu kutoka nyumbani kwao.
Baada ya kufika mtaa wa nne alikuwa tayari ameshafika katika barabara
kuu iendayo Msamvu, vile anaanza tu kukatisha barabara kulitokea
baiskeli
iliyokuwa katika mwendo kasi ilimgonga na kumburuza hadi kwenye
mfereji. Upendo alilalamika sana kwa maumivu makali tumboni na
mgongoni. Wapitaji walisikia mtu akipiga kelele za nisaidieni kutoka
katika
mfereji. Walifika na kumuinua na kumkalisha pembeni mwa barabara.
Wakati wakiendelea kumhoji kilichotokea wale watu waliokuwa wazazi
wake, James, Eliza na watu wengine walifika na kumkuta Upendo akiwa
hoi. Baba yake Upendo alimfukuza James na kutaka asionekane tena
katika
familia ile ilikuwa ni aibu kubwa sana kwani furaha ilileta uchungu.
Upendo alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa
matatibu.
Huko hospitali hali ya Upendo ilizidi kuwa mbaya, mimba aliyokuwa
nayo
iliharibika. Eliza alikuwa karibu naye wakati wote akimwomba msamaha
lakini Upendo alimfariji mdogo wake.
“Usijali mdogo wangu huna kosa mimi ndio mwenye kosa
sikukufahamisha shemeji yako. Lakini vilevile James hakuwa mwaminifu
alikuwa akinidanganya.” Upendo alisema maneno hayo kwa uchungu sana
huku machozi yakimtiririka mashavuni.
Baba na Mama yake Upendo walihuzunika sana wakiwaonea huruma
mabinti zao.
“Wanangu nawapenda sana haya mambo yameshatokea hakuna namna,
yule mwanamume ni muuaji sitaki kumsikia tena, kinachotakiwa ni
Upendo apone maisha yataendelea.” Baba Upendo aliongea huku
akimtazama mkewe.
“Ndio! Wanangu hii ni mitihani ya maisha, ni majaribu ila Mungu
atawasidia.” Mama Upendo aliongeza.
Kadiri siku zilivyokwenda Upendo aliendelea kuumwa sana. James maisha
yalianza kumwendea kombo, alikuwa amechanganyikiwa, siku zote alikuwa
ni mtu wa kujilaumu moyoni mwake akisema.
“Maisha yangu yamebadilika nimemkosa Upendo. Nimemkosea sana
Upendo na Mungu pia sistahili kusamehewa kabisa Mungu nisaidie.”
Aliongea James kwa kukata tamaa kabisa huku wazazi wake wakimwonea
huruma.
Siku moja wazazi wa James waliamua kumshauri James waende hospitali
kumwona Upendo ili akamwombe msamaha kwa mara nyingine.
Walipofika hospitali waliwakuta wazazi wa Upendo pamoja na watoto wao
wote wakiwa wamesimama wamekizunguka kitanda alipolala Upendo.
Walipoingia tu kabla hata hawajasalimia baba yake na Upendo alianza
kuwafukuza.
“Sitaki kuwaona hapa naomba mondoke yaani matatizo yote mnayotupa
hadi sasa bado mnakuja? James nasema ondokeni!” Alitamka baba
Upendo kwa hasira.
“Baba usiwafukuze wakaribishe nataka kuongea na James.” Alitamka
Upendo kwa taabu tena kwa sauti ya chini sana huku akinyoosha mkono
wa kulia akiashiria kumwita James.
“Utaongea naye nini yeye ndiyo chanjo cha wewe kuwa hapa leo nasema
watoke sitaki kuwaona hapa.” Alifoka baba Upendo.
Upendo aliendelea kusisitiza kuongea na James na aliwaomba wote
watoke
nje abaki Eliza na James tu. Wote walitii na kutoka nje huku
wakipigwa
na butwaa kwa nini Upendo amewafukuza.
James aliomba msamaha kwa Upendo akiwa amepiga magoti akijutia yote
aliyoyafanya. Pia James alimwomba msamaha Eliza kwa kumdanganya
kuwa hakuwa na mke wala mchumba. Eliza alimsamehe.
“James nitakusamehe lakini kwa masharti ya kwenda kuishi na mdogo
wangu Eliza mama mtarajiwa wa mtoto wako. Mimi sistahili tena kuwa
mke wako.” Aliongea Upendo huku akimkazia macho James na Eliza.
Kabla James wala Eliza hawajapata nafasi ya kujibu chochote, Upendo
aliyekuwa hoi kitandani aliinuka na kukaa kwa mara ya kwanza tangia
afike
hospitali. James na Eliza walishangaa sana. Eliza pamoja na kushangaa
alifurahi kuona dada yake amekaa, alikwenda haraka nje kuwaita wazazi
wake na ndugu wa James ili waone maendeleo ya ghafla ya afya ya
Upendo.
Huku akiwa amezungukwa na ndugu wa pande zote mbili Upendo
alitabasamu na kugeuka ili kumwangalia kila aliye kuwepo katika
chumba
kile. Kisha Upendo alimshika mkono mdogo wake Eliza pamoja na
mkono wa James.
“Kama nilivyotoa masharti yangu nimekusamehe James, lakini kuanzia
sasa nenda mkaishi kwa furaha na amani na msahau yote yaliyotokea.
Uaminifu iwe nguzo ya upendo katika nyumba yenu. Mkaishi kwa
kumtegemea Mungu katika kila jambo.” Baada ya kuongea hivyo Upendo
akavuta mikono ya wote wawili kuelekea kifuani kwake kisha akaibusu
na
kutamka maneno mawili tu “Nawapenda sana.”
Alipomaliza tu kuongea hivyo ghafla alipatwa na kwikwi na kukohoa kwa
nguvu huku akishindwa kupumua vizuri na kuangukia kitandani huku
akitupatupa miguu na mikono kama mtu mwenye kifafa na ghafla akatulia
na kufumba macho.
Eliza alikwenda haraka kumwita Daktari ambaye alifika na kumpima.
“Upendo amekata roho.” Yalikuwa ni maneno ya Daktari kutokana na
vipimo vyake.
∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞ Mwisho ∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞∞
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.