Pages

Jumanne, Februari 25, 2014

"Wanaume wanaowazuia wake zao kujiunga na vikundi vya ujasiriamali kwa wivu wa mapenzi waache mara moja"

Kitendo cha mwanamke kuacha kujishughulisha na ujasiriamali na kukaa nyumbani inachangia watoto kukosa malezi bora kutokana na kuwategemea Baba zao pekee. Na wanaume ambao wanawanyima wake zao fursa za kujiunga na vikundi vya ujasiriamali waache kwasababu maisha ya sasa yamebadilika hayahitaji kutegemea mzazi mmoja, kwahiyo wanaume waache tabia hiyo kwani mwanamke naye ana haki ya kuwa mjasiriamali ili kuweza kusaidiana katika majukumu ya familia.

 Ni vyema wanaume wakaepukana na mfumo dume wa kutaka kufanya kila jambo la maendeleo wao wenyewe na badala yake wawatumie wanawake katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kwa pamoja waweze kuboresha hali zao na maisha yao. Hayo yamesemwa na Katibu wa Muungano wa Vikundi vya wajasiriamali Manispaa ya Tabora Agnes Maganga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.