Wakati bado kuna utata kuhusu tiba halisi ya ugonjwa wa Ukimwi duniani, wataalamu wamebuni kipira maalumu kinavyowekwa kwenye uke na kuzuia maambukizi ya VVU. Mtafiti Patrick Kiser wa chuo Kikuu cha Evanston, nchini Marekani amesema harakati za kupambana na ugonjwa wa ukimwi zinafanyika kwa hali na mali ili kuwalinda wanawake wasipate maambukizi ya VVU. Anasema "Tatizo kubwa ni pale ambapo mwanamke anapata mwenza ambaye hataki kuvaa mipira ya kiume. Kwahiyo kipira hiki kitamsaidia mwanamke kujilinda na maambukizi.
Kipira hicho kimetengenezwa kwa kuchanganywa na dawa aina mbili tofauti ambazo ni Tenovofir (ya kuzuia maambukizi ya VVU) Na dawa ya kuzuia ujauzito na maradhi mengine ya zinaa. Kipira kikishawekwa kinafanya kazi kama kawaida na huweza kutolewa kwa muda baada ya tendo na baadaye kukirudisha wakati wa tendo. CHANZO MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.