Pages

Ijumaa, Machi 14, 2014

MWANAMKE HUPEVUKA KIAKILI MAPEMA KULIKO MWANAUME


Utafiti umefanyika na kuonyesha licha ya watoto wengi wa kike shuleni kutokufanya vizuri katika baadhi ya masomo kama watoto wa kiume wanasayansi wanasema mtoto wa kike hupata uelewa zaidi mapema kuliko wa kiume. Msemaji wa afya ya Mama na Mtoto Tuzie Edwin kutoka  kituo cha Huduma ya Ushauri Nasaha Lishe, na afya (COUNSENUTH) Amesema  "Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana msichana akili yake huanza kukua  kumzidi mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba pindi wanapolea mtoto wa kike husogea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume. 

Msichana huwa mwepesi katika kuwasiliana na pia huweza kuanza kushirikishwa katika baadhi ya mambo, kama kutumwa dukani mapema zaidi ikilinganishwa  na mvulana, Vile vile msichana anawahi kupevuka ukinganisha na mvulana na ubongo wake hukomaa haraka na hapo ndipo maumbile yake yanapoanza kujitengeneza mapema kwaajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua kwa nafasi kubwa kipindi hiki ukilinganisha na mwanaume ni hadi miaka 10 baadaye. Anasema Edwin.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.