Pages

Alhamisi, Machi 13, 2014

UKATILI MAENEO YA VIJIJINI BADO NI CHANGAMOTO AMBAYO INAHITAJI KUFANYIWA MAPINDUZI.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha haki za binadamu (LHRC), Hellen Kijo Bi Simba anasema pamoja na mwamko wa katika maeneo ya mjini, ukatili katika maeneo ya vijijini bado ni changamoto ambayo  inahitaji kufanyiwa mapinduzi. Baadhi ya ukatili huo ni pamoja na mtoto wa kike kuozeshwa katika umri mdogo, unyanyasaji kwa wajane na ukatili ndani ya familia. Mwanamke bado anachangamoto kubwa kujikomboa. 

 Mapambano yanayohitajika sasa ni kuhakikisha mtoto wa kike anapata nafasi ya kuendelea na masomo yake akijifungua salama. "Akipata ujauzito sheria  imruhusu apate nafasi ya kuendelea na masomo kwani hali ilivyo sasa, jamii nyingi hazijaelimika, mtoto akipata ujauzito basi ataozeshwa hata kwa nguvu" anasema Bi Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.