Alisema mwanamke huyo alitenda unyama huo kwa mumewe majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Ipapa kata ya Ipunga wilayani Mbozi. Mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumkata kisogoni na kitu kinachosadikiwa kuwa ni panga kabla ya kumvunja shingo na mguu wa kushoto. Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi na kuwa kabla ya tukio wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kutuhumiana kuchepuka nje ya ndoa. yao. Mwanamke huyo atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilishwa na kusisitiza kwa kuwataka wanajamii kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha migogoro baina yao badala ya kutumia mabavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.