Pages

Jumatano, Machi 19, 2014

MAHABA NIUE,,,,,,

Mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye, Unaambiwa katika mapenzi unapopenda moyo wako unatakiwa uwe na furaha wakati wote, na usimpende mtu kwasababu fulani, mpende kwasababu unampenda sikuzote mtaishi kwa furaha na amani hata kama mkigombana lazima mtamaliza tofauti zenu kwani kila mmoja anakuwa anamkosa mwenzake na kuona moyo wake unaumia kutokana na kumkosa mwenzake. 

Unaweza kujikuta unahangaika huku na kule lakini moyo wako usitulie kwa sababu pale unapoenda siyo sehemu sahihi kwaajili yako. Wawili wanapopendana kuna vikwazo na changamoto nyingi lakini kama mmependana kiukweli vyote hivyo mnavishinda, kwani majaribu ni sehemu ya maisha. Ndiyo maana unaweza kukuta wapenzi wamegombana, na ikitokea marafiki wakaingilia kati na kutoa ushauri, labda Kwa kumshinikiza mmoja kutengana katika uhusiano huo, lakini mwisho wa siku, baada ya siku mbili tatu unawakuta wale watu wako pamoja wakionekana kuwa na mapenzi motomoto, yaani unabaki umeduwaaa......kiukweli MAPENZI HAYAINGILIWI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.